Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinachonibakisha CUF si Prof. Lipumba-Mbunge CUF
Habari za Siasa

Kinachonibakisha CUF si Prof. Lipumba-Mbunge CUF

Hamidu Bobali, Mbunge wa Mchinga
Spread the love

HAMIDU Bobali, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Lindi amesema kuwa, hatoacha ubunge na kujiunga ACT-Wazalendo alikohamia Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Amesema, hatofanya hivyo kwa sababu hatua hiyo inaweza kusababisha taifa kuingia kwenye hasara ya kurudia uchaguzi na kupoteza fedha nyingi lakini pia hawezi kujizulu kwani atakuwa amesaliti walimpigia kura wake.

Akizungmza leo tarehe 19 Machi 2019 Bobali amesema kuwa, hajabaki CUF kuungana na Prof. Lipumba ili kulinda ubunge wake, bali amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kulinda masilahi ya wapiga kura wake na kuokoa fedha za umma.

“…muda wa kwenda mahakamani haupo, tuachane na habari za kesi turudi kujenga chama chetu,” amesema Bobali nakuongeza; “Natoa rai kwa wabunge wenzangu, madiwani na wenyeviti tusikimbie chama chetu, tuje tujenge chama chetu.”

Katika hatua nyingine, Bobali ameomba radhi uongozi wa CUF na yeyote aliyemkosea ndani ya chama hicho. “Na leo ninautangazia umma na chama, nikiwa mbunge na mwanachama naamini yule niliyomkosea, mwenyekiti atakuwa amenisamehe. Ninachukua fursa hii kuomba radhi wanachama wote na viongozi wa CUF ambao kwa namna moja au nyingine tumekosena.’

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!