April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif: Zitto siyo mnafiki kama yule

Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo, amemweleza Zitto Kabwe kwamba sio mnafiki. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Akikaribishwa Makao Makuu ya ACT-Wazalendo Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Machi 2019 Maalim Seif, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CUF amesema, uamuzi wa kujiunga na ACT-Wazalendo umesukumwa na mambo mengi ikiwemo uimara wa chama hicho na viongozi wake

“Zitto sio mnafiki kama yule (hakumtaja jina). Sio aina ya viongozi anayejikomba kwa wakubwa,” amesema Maalim Seif.

Kwenye mkutano huo uliotumika kumkabidhi kadi ya uanachama wa ACT- Wazalendo Maalim Seif amesema, chama hicho kina viongozi wenye ujasiri, adabu na wanaoendana na mazingira.

Akimwelezea Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amesema, sio kiongozi muoga jambo linalomfanya kuwa kiongozi imara kwa zama hizi.

“Zitto ni mtu makini, ni kiongozi ambaye hasemi jambo bila kufanya utafiti na pale anapomaliza utafiti wake hutoa matamko bila woga wowote,” amesema.

Ameeleza kuwa, kabla ya kufanya uamuzi wa kujiunga na ACT-Wazalendo, walifanya utafiti kwa vyama vine.

“Tulifanya utafiti Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo, tukajiridhisha na kufanya uamuzi wa kuhamia ACT- Wazalendo,” amesema.

Amefafanua kuwa, vyama vyote walivyopita kubisha hodi ili wapokewe vina ubora lakini ACT-Wazalendo waliona ndio kinachowafaa zaidi.

Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo jana terehe 18 Machi 2019.

error: Content is protected !!