Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kwanini twende ACT Wazalendo na sio Chadema?
Makala & Uchambuzi

Kwanini twende ACT Wazalendo na sio Chadema?

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania kupitia Jaji Benhajj Masoud, imeamua kumhalalisha Lipumba (Pro. Ibrahim Lipumba) kama mwenyekiti halali wa CUF.

Sisi tumeendelea kusimamia msimamo wetu kwamba, hatuwezi kufanyakazi na Lipumba na kwa sababu ambazo tumekuwa tukizisema mara kadhaa na ambazo umma umekuwa ukizua kwa mapana yake.

Lakini swali kubwa au hofu kubwa kutoka kwa umma ambao umekuwa unatuunga mkono umekuwa ukituamini kujua tutakwenda wapi.

Na kama tutajiunga na chama tutajiunga na chama gani? Na vyama viwili vikipewa nguvu kubwa zaidi ni ACT-Wazalendo na Chadema na wamekuwepo watu wakitamani tujiunge Chadema.

Kwanza niseme tu, maoni yote ni sahihi kabisa, lakini sisi kama watu ambao nyuma yetu kuna umma mkubwa na tukizingatia sababu za kukataa kufanyakazi na Lipumba pamoja na dhamira ovu ya dola yetu, tuna kila sababu za kufanya uchaguzi sahihi.

Tukijiunga Chadema, maana yake ni kwamba, tutakuwa na chama kimoja cha upinzani chenye nguvu, Bara na Zanzibar na sio viwili au vitatu tena. Maana lengo la adui tangu mwanzo ni kuhakikisha anaua nguvu za upinzani, na haswa vyama viwili Chadema na CUF.

 Na ameshafanikiwa kukiua CUF hivyo kimebaki chama kimoja jambo ambalo kwake anaweza kuwa na fursa kubwa zaidi ya kushughulika na chama kimoja tofauti na mwanzo alipokuwa anashughulika na vyama viwili. Adui yetu atakuwa amefanikiwa.

Tukihamia ACT-Wazalendo ni kweli kwamba, ACT itakuwa chama kipya chenye nguvu kuliko wakati wowote ule. Na hivyo kufanya upinzani kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi na nguvu zaidi.

Kwamba, ACT ambacho kitakuwa na mtaji mkubwa Zanzibar na Bara pia, kitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya siasa na kuimarisha upinzani kwasababu nguvu ileile ya upinzani iliyokuwepo kabla kutokana na uwepo wa vyama viwili vya upinzani Chadema na ACT Wazalendo, havina migogoro ya ndani na vinakuwa kwenye nafasi ya kufanya siasa kikamilifu.

Hivyo lengo la Magufuli kuviua vyama vya upinzani litakuwa limeviimarisha zaidi vyama hivi kuliko wakati mwingine. Watu walewale ambao miaka takrabani miwili tumekuwa kwenye mgogoro usio kwisha, sasa tunakwenda kufanya siasa kimamilifu.

Makala haya imechukuliwa kutoka mitandao

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Prof Mwafenga ulijiamini katika utendaji wako na degree zako 10 – Maige

Spread the loveKIFO cha Prof Hadley Mpoki Mwafenga- Afisa Usimamizi wa Fedha...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hii ndio sura halisi ya Rais Samia

Spread the loveKILA zama na kitabu chake. Hizi ni zama za Rais...

Makala & Uchambuzi

Safari ya Siah Malle katika uhandisi inavyoibua vipaji vipya vya wanawake

Spread the loveSiah Malle ni mfano mzuri wa mwanamke ambaye amefanikiwa kuvunja...

Makala & Uchambuzi

Rekodi ya watalii kuandikwa Desemba 2023

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ifikapo Desemba 2023...

error: Content is protected !!