Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif aendesha kikao mpaka saa 7 usiku
Habari za Siasa

Maalim Seif aendesha kikao mpaka saa 7 usiku

Maalim Seif Sharrif Hamad
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) bado kinapita kwenye tanuri la moto ambapo, Maalim Seif Shariff Hamad, katibu mkuu wa chama hicho jana tarehe 11 Machi 2019 ameendesha kikao mpaka saa 7 usiku. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Maalim Seif ameitisha na kuendesha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Taifa ili kutafakari hatua ya Profesa Ibrahim Lipumba ya kuitisha mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 11 Machi 2019 na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Umma, Mbarala Maharagande, kikao hicho kilianza kufanyika jana tarehe 10 Machi 2019 kuanzia saa 9.00 mchana na kumalizika saa 7 za usiku.

“Maalim Seif ameitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ya taifa kilichoanza saa 9 mchana 10/3/2019 na kumalizika saa 7 za usiku 11/3/2019 kutafakari hatua za kuchukua kutokana na kusudio la Lipumba na genge lake kutaka kukiuka, kupuuza na kuvunja kwa makusudi amri ya zuio ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa tarehe 28 Februari 2019.

“Zuio hilo lilitolewa na Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga kuzuia kuandaa na kuitisha mkutano mkuu wa taifa wa CUF  mpaka pale shauri la msingi namba 84/2018 litakaposikilizwa na kufanyiwa maamuzi,” inaeleza sehemu ya taarifa ya Maharagande.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, kamati hiyo imejadili mambo saba ikiwemo, taarifa ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Joran Bashange iliyoeleza kwamba, chama hicho kimepeleka nakala ya hukumu hiyo kwa vyombo vya dola.

“Ilijadili taarifa za kuwasili Dar es Salaam makundi ya watu kutoka sehemu mbalimbali wanaojipa hadhi ya kuwa wajumbe wa mkutano mkuu pasian kufanyika kwa uchaguzi wa ngazi za tawi, kata na wilaya kwa mujibu wa katiba ya CUF,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, baada ya tafakuri ya kina kamati hiyo imetoa wito kwa wanachama wa CUF, viongozi wa chama, na wapenda demokrasia, kila mmoja kwa nafasi yake kushiriki kuhakikisha amri ya katazo la mahakama kuu linatekelezwa na mkutano wa Prof. Lipumba haufanyiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!