Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa UVCCM wabadili gia kwa Lowassa
Habari za Siasa

UVCCM wabadili gia kwa Lowassa

Spread the love

KEJELI na maneno ya dhihaka yaliyovurumishwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa Edward Lowassa wakati akihamia Chadema, sasa yamebadilika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Leo tarehe 11 Machi 2019, UVCCM imetaka watu wanaomsema Lowassa kwa madhambi yake kwamba, waeleza kama nao hawajachafuka ama hawana dhambi. “… waeleze kama wao hawana dhambi.

Kheri James, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa wakati akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma amewataka wanaohoji hatua ya kupokewa Lowassa, ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu kuacha.

Lowassa muda mfupi baada ya kuondoka CCM na kuhamia Chadema tarehe 28 Julai 2015, miongoni mwa taasisi za CCM zilizomshambulia kwa maneno makali ya dharau, kebehi na kejeli ni UVCCM.

Tarehe 15 Novemba 2015, Kaimu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu alinukuliwa na vyombo vya habari alisema, Chadema kiko kwenye majuto kutokana na uamuzi hasi wa kumkaribisha Lowassa kwa kuwa ni fisadi.

Tarehe 9 Oktoba mwaka 2017 Shaka akiwa kwenye mkutano wa ndani wa UVCCM alisema kuwa, Lowassa hana ndihamu na amepoteza muelekeo na kwamba, ni kama samaki aliyetupa nchi kavu.

‘’…Samaki ukimtoa kwenye maji ukimweka ufukweni ameshapoteza muelekeo, Lowassa ameshapoteza muelekeo.. nani asiyejua kuwa wizi mkubwa uliofanywa ndani ya hii?

“Wao ndio walioingia mikataba ya ovyo wao ndio walioiba ardhi ya nchi hii” alisema Shaka.

Lowassa alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho; katika  uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015, Chadema kikiungwa mkono na jumuiko la vyama vilivyoko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vilimfanya mwanasiasa huyo kuwa mgombea wake wa urais.

Alitangazwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Pombe Magufuli. Hata hivyo, Lowassa mwenyewe amekuwa akidai mara kadhaa kuwa kura zake ziliibwa.

Mbali na Chadema, vyama vingine vilivyomuunga mkono Lowassa, pamoja na Chama cha Wananchi (CUF), NCCR- Mageuzi na National League Democrat (NLD).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!