July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lugola: Kamateni wanaomtukana rais

Kangi Lugola Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Spread the love

KANGI Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ameliagiza Jeshi la Polisi, wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya kuwasweka ndani wanasiasa wataofanya mikutano ya ndani na kumtukana rais. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lugola ametoa agizo holo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kilosa Town, Morogoro.

Amewataka viongozi hao kushirikiana na polisi kukamata wanasiasa wanaofanya mikutano ya ndani na kuvunja sheria za nchi.

Lugola ameelekeza kuwa, wanasiasa hao wachunguzwe wanapofanya mikutano ya ndani kwa kuwa baadhi yao hutumia mikutano hiyo kumtukana Rais John Magufuli pamoja na kutoa kauli zinazochonganisha wananchi na serikali yao.

Amesema, hatomvumilia kiongozi yoyote wa chama cha siasa atakayefanya mikutano ya hadhara au kutumia mikutano ya ndani kukiuka sheria za nchi.

Amewataka wanasiasa kutii agizo la seriali la kutofanya mikutano ya hadhara hadi pale kampeni zitakapoanza katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

error: Content is protected !!