Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Shein ajigamba kupunguza utegemezi Z’bar
Habari za SiasaTangulizi

Rais Shein ajigamba kupunguza utegemezi Z’bar

Spread the love

RAIS wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Shein amesema utegemezi wa fedha katika bajeti ya serikali yake umepungua kutoka asilimia  30 alipoingia madarakani hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka wa fedha wa 2018/19. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Shein amesema hayo leo tarehe 12 Januari 2019, wakati akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya miaka  55 ya mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika kwenye uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

“Utegemezi  katika bajeti wakati naingia madarakani ulikuwa ni asilimia 30.2 Lakini kwa sasa umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka 2018/19 ikilinganishwa na asilimia 7.3 mwaka 2017/18,” amesema Dk. Shein.

Katika hatua nyingine, Dk. Shein amesema ukusanyaji mapato unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) umeongezeka kwa zaidi ya Sh. 100 bilioni, kutoka bilioni 512 mapato yaliyokusanywa mwaka wa fedha wa 2016/17 hadi kufikia Sh. 688.7 bilioni mwaka 2017/18.

Kuhusu kipato cha kila Mzanzibar kwa mwaka, Dk. Shein amesema kipato hicho kimepanda kutoka Sh. 1.8 milioni ambayo ni sawa na dola za Marekani 868 katika mwaka wa fedha wa 2016 hadi kufikia  Sh. 2.2 milioni (dola 914) kwa mwaka 2017.

“Mafanikio hayo yametokeana na juhudi za serikali mbalimbali ikiwemo kuimarisha miundombinu ya kibiashara,” amesema Rais Shein.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!