Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Kipigo cha mvuruga kocha wa JS Saoura
MichezoTangulizi

Kipigo cha mvuruga kocha wa JS Saoura

Spread the love

KIPIGO cha bao 3-0 kutoka kwa Simba, kimemvuruga Kocha Mkuu wa JS Saoura, Nabil Neghiz, hali iliyompelekea kushusha lawama kwa mwamuzi wa mchezo na wanahabari kutoka Tanzania kuwa waliwaondoa mchezoni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kocha huyo alisema kuwa katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, walistahili kupata penalti baada ya mchezaji wake kuangushwa katika eneo la hatari lakini mwamuzi hakufanya hivyo na alionesha dalili zote kuwa upande wa Simba licha ya kukili kuwa wapinzani wake walikuwa vizuri.

“Tulistahili kupata penalti katika mchezo huu lakini mwamuzi hakufanya hivyo, na kuna muda akitunyima kona huenda ingekuwa nafasi kwetu kupata bao katika mchezo wa leo,” alisema kocha huyo.

Aidha kocha huyo akusita kutoa lawama kwa waandishi wa habari wa hapa nchini kwa madai ya kutoa taarifa za upotoshaji kwa kumtafsiri tofauti maneno aliyoongea kwenye mkutano wake na wanahabari hapo jana kuelekea mchezo wa leo.

“Nimesikitishwa sana kuona kutoa tafsiri tofauti ya maneno niliosema jana, eti ya kuwa Simba ni timu dhaifu na haina kocha, eti kwenye kundi hili naziogopa timu mbili tu ambazo ni AS Vita na Al Ahly kutoka Misri, kitu ambacho siyo kweli na mnaonesha picha mbaya kwa jamii,” alisema kocha huyo ambaye alikuwa akiongea kwa kiarabu.

Baada ya matokeo ya leo Simba imefanikiwa kupata alama tatu na kuwa kileleni katika msimamo wao wa kundi D, huku wakitarajia kucheza mchezo wao wa pili dhidi ya AS Vita ya Congo 18 Januari 2019.

Mabao ya Simba katika mchezo wa leo yalifungwa na Emmanueli Okwi dakika ya 45 na Meddy Kagere dakika ya 51 na 57 na hivyo kufanikisha kuchukua alama tatu na leo usiku wanatarajia kusafiri mpaka visiwani Pemba kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC hapo kesho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!