Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Daktari feki mbaroni Dodoma
Habari Mchanganyiko

Daktari feki mbaroni Dodoma

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto
Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mkazi wa Gairo mkoani Morogoro, Hassan Abdallah kwa tuhuma za kufanya kazi ya kitabibu pasipo kuwa na taaluma ya kazi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto amesema Abdallah anayetuhumiwa kuwa daktari feki katika hospitali za wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, alipohojiwa alisema anaipenda taaluma hiyo.

Kamanda Mulloto amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anatoa huduma mbalimbali za upasuaji kwa wagonjwa wenye uvimbe, ambapo alianza kufanya upasuaji huo katika zahanati binafsi

“Tumemkamata akijihusisha na utoaji huduma mbalimbali za kitabibu na upasuaji mdogo kwa wananchi wenye uvimbe, tunaendelea kuchunguza kwa nini anafanya hivyo, tulipomhoji amesema alikuwa anafanya kwenye zahanati binafsi amekuwa akipenda taaluma hiyo ambapo anafanya hivyo pasipo kibali,” amesema Kamanda Muroto.

Kamanda Muroto amesema wanaendelea kumuhoji Abdallah na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

“Tunamhoji tutamfikisha mahakamani. Hatuna nafasi ya utapeli kwenye mkoa wangu udaktari feki hauna nafasi, wananchi watoe taarifa za kutosha,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!