Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lukuvi atumbua watatu Arusha
Habari za SiasaTangulizi

Lukuvi atumbua watatu Arusha

Spread the love

WAZIR wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi watatu wa sekta ya ardhi katika Halmashauri ya Jiji la Arusha. Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).

Maofisa hao wamesimamishwa kazi kwa tuhuma ya kushirikiana na watu wanaotajwa kuwa matapeli wa viwanja katika jiji hilo.

Lukuvi amesema, maofisa hao waliosimamishwa kazi kutokanyaga katika eneo la ofisi za Jiji mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na maamuzi dhidi ya tuhuma zao yatakapotolewa.

Waziri huyo alichukua uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Jiji la Arusha jana kufuatia kuwepo tuhuma nyingi za utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya maofisa wa ardhi wasiokuwa waaminifu kufanya utapeli kwa wamiliki halali wa viwanja.

Maofisa ardhi waliosimamishwa kwa tuhuma hizo za kushirikiana na matapeli kudhulumu viwanja kwa wamiliki halali katika jiji la Arusha ni Elizabeth Mollel, Lassen Mjema na Zawadi Mtafikikolo.

Mbali na kusimamishwa kazi kwa watumishi, pia ameagiza maofisa Ardhi wa jiji Hilo kuhakikisha matapeli wote wa viwanja wanaoshirikiana na watumishi hao wasipatiwe huduma katika masuala yoyote ya ardhi.

Ni kufuatia kuonekana kujihusisha na mipango ya utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha.

Katika ziara yake hiyo ya kushtukiza pamoja na kuelezwa na Ofisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato uwepo wa watumishi wawili Lassen na Zawadi huku Elizabeth akiwa katika likizo ya uzazi, watumishi hao walipotea ghafla ofisini bila taarifa mara baada ya kuelezwa wanahitajika kwa waziri na hata pale walipopigiwa simu za mkononi hazikupatikana.

Kwa mujibu wa Lukuvi, watumishi hao wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na matapeli wa viwanja katika jiji hilo jambo linalotia mashaka utendaji wao wa kazi.

Amebainisha kuwa maofisa hao wamekuwa na tabia ya kufuatilia kesi zilizopo katika Mabaraza ya Ardhi kwa nia ya kuwasaidia matapeli.

Kufuatia kadhia hiyo, Lukuvi ameagiza kuanzia sasa hati zote za wito wa Mahakama nchini kusainiwa na Afisa Ardhi Mteule au Msajili wa Hati ama Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda na Mwanasheria wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi lazima afahamishwe uwepo wa kesi husika.

“Kuanzia sasa summons zote zipokelewe na Maafisa Ardhi Wateule, Makamishna au Wasajili wa Hati wa Kanda na watumishi wengine wasipokee wala kujihusisha” alisema Lukuvi

Amesema matapeli wa viwanja wamekuwa wakifungua kesi katika Mabaraza ya Ardhi dhidi ya wamiliki halali na wakati mwingine matapeli hao hawawafahamu hata wamiliki lengo lao likiwa kuwakatisha tamaa pale kesi inapochukua muda mrefu hasa ikizingatiwa baadhi ya wamiliki hawana uwezo wa kuweka mawakili. Hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza haki zao.

Amesema, tabia hiyo haiwezi kuvumiliwa na kusisitiza kuwa mtandao wote wa matapeli wa viwanja katika jiji la Arusha ataukomesha kama alivyofanya katika jiji la Dar es Salaam ambalo huko nyuma lilishamiri sana kwa tabia hiyo ili kusaidia haki za wanyonge.

Ofisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato alimueleza waziri Lukuvi kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo na wakati mwingine matapeli hao huwashitaki lengo likiwa kujipatia viwanja kwa njia ya udanganyifu na kuviuza.

Lukuvi alifanya ziara hiyo ya kushtukiza katika ofisi za jiji Arusha akitokea wilayani Babati mkoa wa Manyara ambako huko aliweza kutoa faraja iliyopotea kwa muda mrefu kwa wananchi wa vijiji vya Singu na Endasago kwa kuamuru kubaki katika maeneo yao kufuatia mgogoro wa muda mrefu.

Mgogoro huo umedum takriban miaka 50 kati ya wana kijiji na wamiliki wa mashamba ambao ni kampuni za Agric Tanzania Ltd na Endasago Co Ltd.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!