Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliofariki MV Nyerere wafikia 136, Sirro kufanya uchunguzi
Habari MchanganyikoTangulizi

Waliofariki MV Nyerere wafikia 136, Sirro kufanya uchunguzi

Spread the love

IDADI ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere iliyotokea jana tarehe 20 Septemba 2018 imeongezeka kutoka watu 79 hadi 136. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Idadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati akizungumza na wanahabari.

Jana tarehe 20 Septemba 2018 siku ambayo ajali hiyo ilitokea majira ya mchana, miili ya watu takribani 44 iliokolewa kutoka Ziwa Victoria,  huku watu 37 walifanikiwa kuokolewa wakiwa hai.

Zoezi la ukoaji wa miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo linaendelea kufanywa na  Vikosi Maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Sirro amesema watafungua jalada la uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini ukweli wa ajali hiyo ikiwemo chanzo chake.

Baada ya kutokea ajali hiyo, kumekuwepo na tofauti ya idadi ya abiria waliokuwemo kwenye kivuko hicho, huku kukiwepo madai ya kwamba kivuko hicho kilibeba zaidi ya abiria 200, idadi iliyo kubwa ukilinganisha na uwezo wa kivuko hicho wa kubeba abiria wasiozidi 100.

Kivuko cha MV Nyerere kilizama katika Ziwa Victori kikitokea Bugorora kisiwani Ukerewe kuelekea Kisiwa cha Ukara.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

error: Content is protected !!