Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanasheria wa Serikali kuanzisha chama chao
Habari za Siasa

Wanasheria wa Serikali kuanzisha chama chao

Spread the love

SERIKALI ina mpango wa kuanzisha Chama cha Wanasheria walio katika utumishi wa Umma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mpango huo umeelezwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi katika mkutano wa siku mbili wa Mawakili wa Serikali walio  katika utumishi wa umma unaofanyika jijini Dodoma.

Dk. Kilangi wakati akiwasilisha mada kuhusu  Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa  Mawakili wa Serikali walio  katika utumishi wa umma amesema,  anakusudia  kuanzisha Chama cha Wanasheria walio  katika utumishi wa Umma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kwamba, kuanzishwa kwa  Chama hicho ni kwa mujibu wa  Ibara ya 74 ya  Muswaada wa  Sheria ya  Marekebisho  Mbalimbali ( Na.2) 2018  inayoeleza kuwa , “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali  anaweza  kuanzisha Chama cha Wanasheri katika Utumishi wa Umma”.

Aidha, amesema kuanzishwa kwa  chama cha Mawakili  wa Serikali walio katika utumishi wa Umma hakutawanyima fursa mawakili hao ya  kujiunga au kuwa wanachama wa  vyama  vingine vya kitaaluma kikiwamo Tanganyika law Society ( TLS).

Kuhusu majukumu ya kuitendaji ya chama hicho, Dk. Kilagi ameeleza kuwa Chama hicho kitakuwa  kinakutana  mara moja kwa mwaka kwaajili ya  kujadili masuala mbalimbali ya kisheria ikiwamo  maendeleo ya taaluma hiyo na au kuitishwa na waziri wa katiba na sheria.

Vile vile, amesema Waziri atatunga  Kanuni kuhusu  usimamizi, uongozi, muundo na uendeshaji wa shughuli za chama pamoja na kupokea ripoti ya mikutano ya chama hicho .

Mawakili hao wa Serikali  wapatao mia tisa ( 900) wanatoka  Wizara mbalimbali,  Idara za Serikali, Taasisi na  Mashirika yanayojitegemea, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mkutano huo  ambao  ni wa pili kufanyikia ulifunguliwa na  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!