Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli ammaliza kabisa Makonda
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli ammaliza kabisa Makonda

Spread the love

RAIS  John Magufuli amefunga mjadala kuhusu makontena 20 yenye samani ikiwemo meza na viti yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kukwama katika bandari kavu ya mkoa huo kutokana na kudaiwa kodi ya kiasi cha Sh. 1.2 bilioni. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Makontena hayo yenye samani mbalimbali, yaliingizwa nchini na Makonda kwa ajili ya kile kilichoitwa itwa kutolewa kama msaada kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika   mkutano wake na madiwani, viongozi pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo tarehe 30 Agosti 2018, Rais Magufuli amesema kuwa, kwa mujibu wa sheria za nchi mtu mmoja tu ndiye anayeruhusiwa kupokea misaada pasina kutoa kodi, na kutaka watumishi wa umma wasitumike kwa masilahi ya watu fulani.

“Lazima viongozi no matter uko kwenye position gani  (hata kama uko kwenye nafasi gani) tujenge mazingira ya kuwatumikia watanzania, eti nasikia sadaka ya jiji la Dar es Salaam mkuu wa mkoa ameleta makontena anaambiwa alipe kodi kwa nini asilipe kodi?” amehoji Rais Magufuli.

Dk. Magufuli ameongeza kuwa “ Kwa sababu katika sheria za nchi yetu kwa mfano ni mtu mmoja tu katika nchi hii aliyepewa dhamana kwa mujibu wa sheria, sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya dhamana  na misaada kupitia sheria namba 30 ya mwaka 1974 mtu huyo ndiye amepewa dhamana ya kupokea misaada kwa ajili ya nchi hakuna mtu mwingine.”

Rais Magufuli ameonyesha wasi wasi wake juu ya sababu za ujio wa makontena hayo akisema kuwa, kitendo cha kutokuwepo kwa orodha ya majina ya shule husika zilizolengwa kupatiwa msaada huo, akisema kuwa kinaweza kutumika kama kichaka cha ukwepaji kodi.

“Sasa ukichukua makontena kule umezungumza labda na watu wengine au wafanyabiashara unasema una makontena yako halafu unasema ya walimu wala hata shule hazitajwi maana yake nini? Maana yake si unataka utumie waalimu ulete hayo makontena upeleke shule mbili tatu ndizo zitapewa mengine utapelekea kwenye shoping. Wafanyakazi wasitumike kwa masilahi ya watu fulani,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!