Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Makapu afiwa na mama yake mzazi, aachwa Dar
Michezo

Makapu afiwa na mama yake mzazi, aachwa Dar

Said Juma Makapu, kiungo wa Yanga
Spread the love

SAID Juma Makapu amefiwa na mama yake mzazi nyumbani kwao Zanzibar, hivyo kusababishwa kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa Yanga wanaosafiri kuelekea nchini Rwanda katika mchezo wao dhidi ya Rayon Sports utakaochezwa Jumatano ya tarehe 28, 2018 wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Anaripoti Halidi Mhina … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga imeeleza kuwa msiba huo umetokea jana na mazishi yanatarajiwa kufanyik leo saa 7 mchana, nyumbani kwao Zanzibar.

Klabu ya Yanga imempa mapumziko Makapu kwenda kushuhurikia taratibu za kumpuzisha mama yake mzazi na baadae atarejea kujiunga na kikosi cha chake katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga inashika mkia katika kundi D, ikiwa na pointi nne tu, nyuma ya Rayon yenye pointi sita, wakati Gor Mahia na USM Alger kila moja ina pointi nane na zinamenyana kwenye mechi ya mwisho Jumatano pia mjini Algiers.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!