SAID Juma Makapu amefiwa na mama yake mzazi nyumbani kwao Zanzibar, hivyo kusababishwa kuondolewa katika orodha ya wachezaji wa Yanga wanaosafiri kuelekea nchini Rwanda katika mchezo wao dhidi ya Rayon Sports utakaochezwa Jumatano ya tarehe 28, 2018 wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Anaripoti Halidi Mhina … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga imeeleza kuwa msiba huo umetokea jana na mazishi yanatarajiwa kufanyik leo saa 7 mchana, nyumbani kwao Zanzibar.
Klabu ya Yanga imempa mapumziko Makapu kwenda kushuhurikia taratibu za kumpuzisha mama yake mzazi na baadae atarejea kujiunga na kikosi cha chake katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga inashika mkia katika kundi D, ikiwa na pointi nne tu, nyuma ya Rayon yenye pointi sita, wakati Gor Mahia na USM Alger kila moja ina pointi nane na zinamenyana kwenye mechi ya mwisho Jumatano pia mjini Algiers.
Leave a comment