December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Basila aahidi zawadi ya uhakika kwa mshindi

Basila Mwanukizi, Mkurugenzi wa kampuni ya Look LTD (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

BASILA Mwanukizi, Mkurugenzi wa kampuni ya Look LTD ambao ni waandaaji wapya wa Shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2018 amesema kuwa atahakikisha mshindi anapata zawadi ya gari inayostahili. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Mwanukuzi amesema hayo ikiwa hivi karibuni katika Shindano la Miss Lake Zone walikataa zawadi ya gari alilopewa nshindi huyo kwa kigezo cha kuwa halikustahili kupewa mrembo.

“Mrembo wa mwaka huu atapata gari zuri kabisa lakini ni vizuri ukampa gari zuri au usimpe gari kuliko kumpa gari ambayo ipo chini ya kiwango, ndiomaana gari ya kwenye mashindano ya Lake Zone tuliikataa kwasababu tuliona lazima tuwathamini warembo wetu, tumejiandaa vizuri na mrembo wetu atapata gari zuri tu na mtaliona,” amesema.

Hata hivyo Mwanukuzi amesema kuwa wao kama waandaaji wanahakikisha mambo kama ushindi kwa rushwa ya ngono, uvaaji ambao sio utamaduni wa kitanzania pamoja na mambo mbalimbali ambayo hayaleti picha nzuri katika tasnia hiyo ya urembo yanatoweka ili kurudisha hadhi ya shindano hilo.

“Sisi wote tubadilishe fikra tusirudi kwenye malalamiko na changamoto za nyuma tutakuwa hatusongi mbele, sisi ni kampuni mpya tupeane muda ili tuulizane changamoto zetu sisi kwakuwa hatuwezi kuzijibia changamoto zilizokuwa chini ya waandaaji wengine,” amesema.

error: Content is protected !!