SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteuwa Ammy Ninje kuwa Kocha Mkuu wa muda wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 20, ‘Ngorongoro Heroes’ ambayo inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya dhidi ya Morocco na Msumbiji. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Ninje ambaye hapo awali alikuwa kocha wa muda wa Timu ta Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ iliyoshiriki michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika nchini Kenya katika mwaka uliopita na kuondoshwa katika hatua ya makundi.
Ngorongoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi ya Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha huyo ataiongoza Ngorongoro Heroes katika michezo hiyo miwili ya kirafiki kabla ya kuivaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 (AFCON U20).
Mchezo huo ambao utachezwa Machi 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na mechi ya marudiano itafanyika baada ya wiki mbili mbili jijini Kinshansha, nchini Congo.
Leave a comment