Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Switzerland yawakumbuka walemavu
Habari Mchanganyiko

Switzerland yawakumbuka walemavu

Spread the love

WATU wenye ulemavu nchini wameiomba serikali  na taasisi mbalimbali binafsi kuwasaidia  eneo la   kujenga ofisi ya kudumu. Anaandika Angela Willium

Wamesema wanahitaji ofisi kwa kuwa hivi sasa sehemu wanayotumia wameazimwa kwa muda na Msikiti wa Membe Chai uliopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,  Mwenyekiti wa Taasisi  ya Walemavu ijulikanayo kama MITWE, Habibu Hamimu amesema tatizo hilo la kukosa ofisi wamekuwa nalo kwa muda mrefu sasa.

Aliyasema hayo wakati akipokea msaada wa viti vya walemavu na baiskeli kutoka Taasisi ya Furaha ya Switzerland.

“Tunaiomba serikali na wana  jamii watusadie eneo la kujenga ofisi ya kudumu  kwani hapa tulipo ni jengo la Msikiti wa   Mwembechai ambayo hata hivyo  hiyo inavuja kipindi cha mvua na misaada tuyopokea ni mikubwa ikilinganisha na ofisi tuliyo nayo, ” amesema Hamimu

Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho  wilaya ya Kinondoni,   Saidi Machaku amesema walemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo suala la afya.

“Wazazi au walezi wanao ishi na watu wenye ulemavu tuna waomba muwe mna waleta walemavu wenzetu katika kupokea misaada badala ya kuwafungia ndani na hapa kuna mlemavu mmoja sijamuona nahisi wazazi hawajamleta kwa kuwa wanaona aibu kuja naye, ” amelalamika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

error: Content is protected !!