Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Takukururu yamgeuzia kibao Mbunge Nassari
Habari za SiasaTangulizi

Takukururu yamgeuzia kibao Mbunge Nassari

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari
Spread the love

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemugeuzia kibao Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari  (Chadema)  ambaye amewapelekea ushahidi wa namna Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti alivyotumia rushwa kuwashawishi Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukihama chama hicho, anaandika mwandishi wetu.

Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi kwamba  taasisi hiyo ingeufanyia kazi ushahidi uliowasilishwa kwao na Mbunge huyo, lakini leo imemuonya mwanasiasa huyo na kumtaka asitoe aina yoyote ya shinikizo baada ya kuwapa ushahidi.

“Hii Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu tutachukua hatua za kisheria dhidi  yake”

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola, ametoa onyo hilo leo na kusisitiza kuwa hawafanyi kazi kwa shinikizo la mtu.

Nassari akiongozana na wabunge kadhaa wa Chadema wameiwasilisha ushahidi huo wa video kwa TAKUKURU ili iweze kufanya uchunguzi wake kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!