Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lema: Rais Magufuli amedanganywa na wasaidizi wake
Habari za SiasaTangulizi

Lema: Rais Magufuli amedanganywa na wasaidizi wake

Wabunge wa Chadema, Mch. Peter Msigwa (wa kwanzakushoto), Godbless Lema na Joshua Nassari
Spread the love

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema kuwa Rais John Magufuli amedanganywa na wasaidizi wake kuhusu suala la kujiuzulu kwa madiwani wa Chadema kuwa wamemuunga mkono kazi yake ilhali walishinikizwa na Rushwa, anaandika Faki Sosi.

Wabunge hao Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, Joshua Nassari, Arumeru Mashariki na Mch: Peter Msigwa wa Iringa Mjini ambao walifika Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kupeleka ushahidi wa vitendo vya rushwa walivyodai kufanywa na Mkuu wa ya Arumeru Alexander Mnyeti.

Wabunge hao wamedai kuwa rushwa zilitumika kuwashawishi madiwani hao kukihama Chadema, lakini taarifa ilitolewa kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli.

Leo majira ya saa 9 alasiri wabunge hao waliwasili katika ofisi za Takukuru na kutoka saa 10 kisha kuzungumza na waandishi wa habari.

Lema amesema kuwa rais amedanganywa na wasaidizi wake na kwamba hatoweza kuvumilia kitendo hicho badala yake atachukua hatua.

“Si kweli kuwa watu wanaacha udiwani kwa sababu ya kuunga mkono kazi ya Rais, isipokuwa Rais alidanganywa na wasaidizi wake. Ukweli ni kwamba rushwa imetumika kuwashawishi madiwani hao.

“Tunaamini hili jambo litakuwa limemkera Rais na tunaamini kwamba atachukua hatua za haraka wakati watu hawa wanachunguzwa,” amesema Lema.

Amesema kuwa wamepokelewa vizuri na Mkurugenzi wa Takukuru, Valentino Mlowola pamoja na timu yake ya uchunguzi na kukubaliana mambo ya msingi pamoja na kumkabizi sehemu ya ushahidi.

Amesema kuwa Takukuru wamewahakikishia kuwa watafungua jarada rasmi la tuhuma hizo pamoja na kuwatoa wasiwasi kuwa Taasisi hiyo ipo huru kufanya uchunguzi wa hata tetesi zinazohusiana na rushwa.

Nassari amesema kuwa wanaushahidi usiokuwa na shaka kuhusu madiwani waliokuwa wamejiuzuru kwamba hawajajiuzuru ili kumuunga mkono Rais isipokuwa wameuunga mkono rushwa.

Amesema kuwa hakuna shaka yoyote kuhusu video hizo na kwamba sio kama zinavyodaiwa kuwa zimerekodiwa mwaka 2008 isipokuwa ilikuwa ni hitarafu za kamera iliyotumika ndio zinaonyesha hivyo.

Amesema kuwa mwaka 2008 wahusika kwenye video hiyo hawakuwa kwenye nafasi waliyokuwa nayo saa hivi akitoa mfano Mkuu wa Wilaya Mnyeti hakuwa Mkuu wa wilaya na wengine walikuwa Chuoni wakisoma.

Mchungaji Msigwa amesema kuwa uchunguzi huo wameufanya kwa vifaa kutoka Uingereza na kwamba upo muendelezo wa video zilizorekodiwa wakati vitendo hivyo vya rushwa vikiendelea.

Amewataja wakuu wa wilaya pamoja baadhi ya askari wa jeshi la polisi waliohusika kwenye vitendo hivyo pamoja na kuweka wazi kuwa vitendo hivyo vimetokea na jimboni kwake na kwamba Mkuu wa Mkoa wa Iringa amehusika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

error: Content is protected !!