Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Watu wasiojulikana wafungua matairi gari la Lema
Habari MchanganyikoTangulizi

Watu wasiojulikana wafungua matairi gari la Lema

Spread the love

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema watu wasiojulikana walifungua baadhi ya nati kwenye taili ya gari yake kitu ambacho kingeweza kumsababishia ajali, anaandika Hamis Mguta.

Lema na Mbunge wa Arumeru mashariki (Chadema), Joshua Nassari walipanga kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema ambapo kabla ya kuanza safari walibaini kuwapo kwa tatizo kwenye gari.

“Juzi nilisikia sauti isiyosawa tairi za nyuma nikapaki gari Equator Hotel. Dereva alipochukua gari tairi zote zikachomoka. Ninalindwa na Mungu.

“Tulibaini tairi za mbele wamefungua wakaacha wheelnut mbili mbili kila tairi, nyuma waliacha moja upande wa kushoto na kulia wakaacha mbili,” aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Amesema kuwa baada ya kuhisi tatizo hilo aliliegesha katika hoteli ya Equator na baadaye kuomba msaada kwenye gari la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es Salaam.

“Asubuhi leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka,” amesema.

Amesema tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba kampuni ya ulinzi ya Inteligence inayolinda nyumba yake kufanya uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!