Saturday , 9 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Chadema Morogoro  waangusha maombi kwa Lissu
Habari Mchanganyiko

Chadema Morogoro  waangusha maombi kwa Lissu

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, akilia kwa uchungu
Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati pamoja na uongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro wameungana kufanya maombi ya kumwombea mbunge wa Singida Mashariki ,  Tundu Lissu pamoja na kuhamasisha michango kwa ajili ya matibabu.

Maombi hayo  yalifanywa na uongozi wa kanda ya  kati pamoja na uongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro   huku wakilaani  vitendo vya  polisi kuendelea  kuwakamata na kuwanyanyasa wapinzani.

Viongozi hao wa Chadema wamesema polisi wameshindwa kuwakamata ama kutoa taarifa za watu ambao wanafanya uhalifu lakini hawabainiki.

Awali viongozi hao wa chadema kanda ya kati pamoja na mkoa Morogoro walikutana kwa lengo la kuweka uongozi wa Chadema msingi ambao utafanya kazi ya kuratibu shughuli zote za kuimarisha chama ikiwa ni pamoja na kukijenga.

Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa Chadema kanda ya kati,  Alphonce Mbassa amesema kuwa licha ya kuwepo changamoto kubwa ya kufanya siasa kwa sasa kutokana na serikali kwa kutumia vyombo vya dola kuukandamiza upinzania, lakini ni lazima chama kiweke mikakati ya kuimarisha.

Akizungumzia kuhusu suala la  polisi kuwakamata viongozi wakiwa katika shughuli zao za kawaida,  Mbassa amesema umefika wakati wa wanachama kutambua kwamba wanatakiwa kutumia nafasi zao kufanya siasa bila kuwa na uoga.

“Nataka niwaeleze viongozi na wapenzi wa Chadema kanda ya kati, mkoa wa Morogoro pamoja na taifa kwa ujumla, wote mnajua kuwa kiongozi wetu Tundu Lissu alipigwa risasi,  lakini imekuwa shida sana kuandaa maombi, kuvaa tishert ni shida hata kufanya  michango imeoneekana kuwa ni jambo la kisiasa.

“Mkiona hali kama hiyo sasa hapo ndo pakujua kuwa serikali inaelekea kuanguka na vyama vya upinzani kuchukua dola” amesem Mbassa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!