Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kumburuza DC Chemba mahakamani
Habari za Siasa

Chadema kumburuza DC Chemba mahakamani

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Chemba, Dodoma, umejipanga kwenda mahakamani kumfungulia kesi Mkuu wa Wilaya hiyo Samson Odunga, anaandika Dany Tibason.

Kusudio la kwenda mahakamani kumfungulia keshi linatokana na madai ya kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji cha Chemka, Hussein Katikilo (Chadema) bila sababu za msingi.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Chemba, Salia Palangyo amesema chama kinafanya utaratibu wa kwenda mahakamani kupinga kitendo cha mkuu wa Wilaya Kumwondoa madarakani mwenyekiti huyo kinyume na utaratibu.

Amesema kwa sasa kumezuka mtindo wa wakuu wa wilaya kuwasimamisha wenyeviti wa mitaa au vitongoji wanaotokana na vyama vya upinzani kinyume na taratibu zinazotakiwa kufuatwa na kudai kuwa hizo ni njama za kutaka kudhoofisha upinzani.

Palangyo amesema kitendo cha mkuu wa wilaya kuitisha mkutano na kutangaza kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji bila utaratibu kamwe hakiwezi kukubalika na lazima kipingwe.

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho, Katikilo amesema kuwa imemshangaza kuona mkuu wa wilaya mzima akiitisha mkutano kishabiki na kutangaza kumvua madaraka yake ya uenyekiti.

Amesema baada ya serikali kutangaza kutenga maeneo ya malisho halmashauri kuu ya kijiji iliamua kutenga maeneo ya malisho na kukubaliana wote na kupeleka suala hilo katika mkutano mkuu na kuridhia.

Amesema kuwa baada ya kulidhia kuwa eneo hilo liwe sehemu ya malisho walijitokeza watu wachache ambao walikaidi na kuanza kulima katika eneo hilo lililokuwa limetengwa kupitia malisho ya mifugo.

Amesema watu hao walionekana kufanya vurugu pale ambapo walizuiliwa na kupeleka malalamiko kwa mkuu wa wilaya ambaye amefanya maamuzi bila kufuata busara za kiuongozi.

Hata hivyo amesema mkuu wa wilaya ya Chemba hakuweza kutumia kanuni zinazoongoza utendaji katika serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kwani yeye aliitisha mkutano na kwa kutumia ilani ya CCM na kuwataka wananchi wapige kura wenye imani na mwenyekiti na wasiokuwa na imani na mwenyekiti.

“Tunajua kuwa sasa serilikali ya CCM imejipanga kuua upinzani lakini tutafuata sheria,” amesema Katikilo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Chemba, Samson Odunga amesema kuwa yeye alifuata taratibu zote za kumwondoa mwenyekiti kwani wanaopiga kura ya kutokuwa na imani na kiongozi wao ni wananchi wenyewe.

Amesema baada ya wananchi kumpelekea malalamiko ya mwenyekiti wao yeye aliitisha mkutano na wananchi walipiga kura ya kutokuwa na imani naye na ndiyo njia ya kumwondoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!