TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amemuwakia William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema baada ya kurudisha fedha za Escrow zinazodaiwa kutakatishwa, anaandika Irene Emmanuel.
Lissu amedai kuwa, Ngeleja ni sehemu ya mafisadi wanaotumia madaraka vibaya hivo anatakiwa kushtakiwa pamoja na wengine wote walionufaika na pesa hizo, kurudisha fedha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) si suluhu kwani sio hao waliompatia fedha hizo apo awali.
Ameeleza kuwa, kutokana na maelezo yake yanaonyesha yeye ni mla rushwa na muongo, sakata hilo ni la muda mrefu sasa na si kama amejua juzi.
“Kusema alijua juzi kuwa fedha hizi ni kashfa, ni kutundanganya, anatakiwa kukamatwa na kushtakiwa,” amesema Lissu na kuongeza: “Nchi hii ukikamatwa umeiba ndiyo kesi imeishia hapo?Sheria ni kuwa ukikamatwa umeiba unafikishwa kwenye vyombo vya dola ukakutwa na hatia unafungwa na fedha kurudishwa.”
Aliongeza kuwa, wote walionufaika na fedha hizo wanapaswa kuwajibishwa na kumtaka rais achukue hatua kuanzia aliyeruhusu fedha hizo zitoke, kwani naye analeta maswali mengi.
Ngeleja aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge na kuondolewa mwaka 2014 baada ya sakata hilo, na juzi ameripotiwa kurudisha fedha TRA alizopewa na James Rugemalira, fedha zinazodaiwa kutakatishwa.
Leave a comment