Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mashine ya kuzalisha mkaa wa kutengeneza yazinduliwa
Habari Mchanganyiko

Mashine ya kuzalisha mkaa wa kutengeneza yazinduliwa

Leonard Gabriel, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka
Spread the love

KAMPUNI ya Kuja na Kushoka Tools Manufactures Group kimezindua mashine ya kutengeneza mkaa unatokana na taka na kukaushia zao la tumbaku, anaandika Irene David.

Leonard Gabriel, Mkurugenzi wa kiwanda hicho amesema ili kukomesha tatizo la kuharibu mazingira na ukame wametengeneza mashine hiyo ili kuwasaidia Watanzania hasa wakulima wanaweza kutumia mkaa huo kuepuka matatizo hayo.

“Tumekuja na ubunifu wa mashine yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mkaa mbadala, yenye uwezo wa kuzalisha mkaa kilo 160 kwa saa na kuzalisha gunia zisizopungua 20 hadi 30 kwa siku,” amesema Gabriel.

Gabriel amesema njia mbadala ya kupata mkaa na wenye bei nafuu itakayomwezesha kila Mtanzania wa kawaida kumudu.

Amesema, mtambo huo mbali na kutengeneza mkaa kwa kutumia taka pia inaweza kutumika kwa kukaushia zao la tumbaku, hivyo ameiomba serikali kutamka kwa sheria kwa kila mkulima wa tumbaku kuanza kutumia tekinolojia hiyo katika ukaushaji.

“Mtambo huu pamoja na kuzuia kabisa matumizi ya kuni kukausha tumbaku pia utaongeza thamani ya mazao kwani mabaki yote ya mazao yatakuwa malighafi,” amesema Gabriel.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!