Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu amchongea Ngeleja Takukuru
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu amchongea Ngeleja Takukuru

Tundu Lissu, Rais wa TLS
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amemuwakia William Ngeleja, Mbunge wa Sengerema baada ya kurudisha fedha za Escrow zinazodaiwa kutakatishwa, anaandika Irene Emmanuel.

Lissu amedai kuwa, Ngeleja ni sehemu ya mafisadi wanaotumia madaraka vibaya hivo anatakiwa kushtakiwa pamoja na wengine wote walionufaika na pesa hizo, kurudisha fedha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) si suluhu kwani sio hao waliompatia fedha hizo apo  awali.

Ameeleza kuwa, kutokana na maelezo yake yanaonyesha yeye ni mla rushwa na muongo, sakata hilo ni la muda mrefu sasa na si kama amejua juzi.

“Kusema  alijua juzi kuwa fedha hizi ni kashfa, ni kutundanganya, anatakiwa kukamatwa na kushtakiwa,” amesema Lissu na kuongeza: “Nchi hii ukikamatwa umeiba ndiyo kesi imeishia hapo?Sheria ni kuwa ukikamatwa umeiba unafikishwa kwenye vyombo vya dola ukakutwa na hatia unafungwa na fedha kurudishwa.”

Aliongeza kuwa, wote walionufaika na fedha hizo wanapaswa kuwajibishwa na kumtaka rais achukue hatua kuanzia aliyeruhusu fedha hizo zitoke, kwani naye analeta maswali mengi.

Ngeleja aliwahi kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge na kuondolewa mwaka 2014 baada ya sakata hilo, na juzi ameripotiwa kurudisha fedha TRA alizopewa na James Rugemalira, fedha zinazodaiwa kutakatishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!