Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Simbachawene awaonya ma-DC, ma-RC
Habari Mchanganyiko

Simbachawene awaonya ma-DC, ma-RC

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene
Spread the love

GEORGE Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amesema wakuu wa wilaya na mikoa wanatakiwa kuacha kufanya mambo yaliyo nje ya mipaka ya kazi zao kwa mujibu wa sheria, anaandika Dany Tibason.

Simbachawene ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa malalamiko kuhusu Christiana Mndeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye anadaiwa kuvuka mipaka ya kazi zake.

Masoud Abdalah Salim, Mbunge wa Mtambile (CUF) amemshutumu Mndeme kwa kutumia magenge ya watu wenye nia mbaya ili kumsimamisha Ismail Seif, Mwenyekiti wa mtaa wa Mlimwa Kusini (CUF).

“Nataka kusikia kauli ya serikali ni hatua gani zitachukuliwa kwa DC huyu kwani ameacha majukumu yake na kushirikiana na watu wenye nia mbaya na kumtengenezea mizengwe mwenyekiti wa mtaa na kumuondoa katika nafasi yake wakati wananchi waliompigia kura bado wanampenda?” amehoji.

Waziri Simbachawene amesema ni makosa kwa wakuu wa wilaya na mikoa kutumia vibaya madaraka waliyonayo na kuwataka wazingatie sheria ambayo ndiyo inawaongoza katika kazi.

“Sheria inayowaongoza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya inawaelekeza kufanya kazi bila kuvuka mipaka yao na hawatakiwi kufanya kazi kwa kutumia mabavu au kwa kuonesha chuki ya wazi,”amesisitiza Simbachawene.

Amesisitiza sheria na taratibu za kazi lazima zizingatiwe na kila kiongozi wa umma na kwamba ni vyema wakuu wa mikoa na wilaya wakawa makini wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Katika hatua nyingine Naghenjwa Kaboyoka, Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki (Chadema), ameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka za kupeleka walimu katika shule ya msingi ya Bwambo Changuruwe yenye walimu wawili tu huku ikiwa na wanafunzi.

“Kwa kuwa suala la elimu ni suala zito na nyeti zaidi, na kwa kuwa elimu inatakiwa kwa kila mtanzania je ni hatua gani ambazo srikali inachukua kupeleka walimu katika shule ya msingi ya Bwambo-Changuruwe ambayo ina walimu wawili huku wapo wanafunzi 250.

“Serikali itueleze, inawezekanaje shule yenye wanafunzi 250 ikawa na walimu wawili tu tena kwa muda mrefu sana, Je kwa hali hiyo serikali ina nia njema ya kukuza elimu nchini?” alihoji Kaboyoka.

Akijibu swali hilo Selemani Jafo, Naibu Waziri wa Tamisemi amesema, pamoja na uhaba wa walimu lakini si sahihi shule hiyo kuwa na walimu wawili tu huku wanafunzi wakiwa wengi.

Amemuagiza Ofisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha anapeleka walimu katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kupatiwa elimu yenye ubora.

“Suala la walimu katika mkoa wa Kilimanjaro si tatizo kubwa, walimu wengi wapo mjini, kutokana na hali hii ambayo Mhe. Kaboyoka amesema naagiza ofisa elimu Mkoa apeleke walimu katika shule hiyo haraka iwezekanavyo,” amesema Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!