Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ole Sosopi atupwa rumande
Habari za Siasa

Ole Sosopi atupwa rumande

Patrick Ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) akiwa jukwaani
Spread the love

PATRICK Ole Sosopi, makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, akituhumiwa kufanya mkusanyiko usio na kibali, anaandika Charles William.

Sosopi amehifadhiwa mahabusu ya kituo kikuu cha polisi manispaa ya Iringa, baada ya kujisalimisha leo leo Jumatatu kufuatia agizo lililotolewa na Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai – mkoa wa Iringa (RCO).

Sosopi aliamriwa kujisalimisha ofisini kwa RCO wa Iringa, ili kuhojiwa, akikabiliwa na tuhuma za kufanya mkusanyiko usio na kibali mnamo tarehe 16 Juni, 2017 katika Kata ya Mlenge, Pawaga Jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Jackson Mnyawami, Katibu wa Bavicha mkoa wa Iringa akizungumzia kukamatwa kwa Sosopi amesema, “Tumefanikiwa kukutana na RCO wa Iringa, tunezungumza naye kwa kwa zaidi ya saa moja lakini amesema Sosopi hawezi kupewa dhamana leo.

“RCO amedai kuwa Sosopi ni kiburi, wameshamuonya mara kadhaa lakini anaendelea na mikutano. Amesema lazima wamlaze mahabusu mpaka kesho na kwamba kama tunataka kumdhamini tuende kesho asubuhi.”

Hii ni mara ya tatu kwa jeshi la polisi mkoani Iringa kumkamata Sosopi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi. Juni mwaka jana, lilimkamata na kumsafirisha mpaka jijini Dar es Salaam, akituhumiwa kwa uchochezi, hata hivyo alihojiwa tu, hakufikishwa mahakamani.

Sosopi ni hasimu mkubwa wa kisiasa wa William Lukuvi, Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Sosopi alitoa upinzani mkali kwa Lukuvi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!