Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Simbachawene awaitia fulsa watu Dodoma
Habari Mchanganyiko

Simbachawene awaitia fulsa watu Dodoma

Jengo la Bunge la Tanzania mjini Dodoma
Spread the love

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kimaendeleo zinazopatikana katika mkoa wa Dodoma kutokana na uwepo kwa makao makuu, anaandika Dany Tibason.

Mbali na kuwataka kuchangamkia fursa kiongozi huyo, amewataka wananchi kuacha tabia ya kubweteka na kusubiria misaada kutoka kwa wafadhili.

Alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Benki ya  DCB Commercial Bank uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF mjini Dodoma.

Simbachawene amesema ili kuondokana na umasikini ni vyema kila mtanzania kuhakikisha anafanya kazi huku wakichangamkia fursa ambazo zinatokana na taasisi za kibenki.

Kutokana na Dodoma kuwa makao maku ya nchi kuna kila sababu ya kutumia taasisi za kifedha kwa ajili ya kuomba mikopo kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi.

“Lazima Dodoma ipewe kipaumbele ya kujiendeleza kiuchumi na mfano mzuri sasa ni kuitumia benki ya DCB  abayo kwa sasa imezinduliwa rasm katika mkoa wa Dodoma kutoka na umuhimu Dodoma kuwa makao makuu.

Akizungumzia DCB aliwataka wananchi kujiunga na benki hiyo ili kuweza kufungua akaunti ili kuweza kupata mkopo kwa masharti nafuu pamoja na kutoza riba kidogo ambayo ni miatano kwa mwezi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Benki ya DCB,Edson Mkwawa amesema bnki hiyo inalenga kuwakomboa wananchi ili kuhakikisha wanapata mikopo ya riba nafuu kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Amesema ili wananchi waweze kuondokana na umasikini ni jambo jema wakajiunga katika vikundi pamja na kukopa mikopo kwa riba nafuu zaidi kwa lengo la kujiongezea kipata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!