Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya vyeti feki yamlinda Makonda
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti ya vyeti feki yamlinda Makonda

John Magufuli, Rais wa Tanzania (katikati) akikabidhiwa ripoti ya Uhumishi na Waziri wake, Angellah Kairuki (kulia)
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye anatuhumiwa kutumia vyeti feki amenusurika kuondolewa katika nafasi yake baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kutangaza kuwa ripoti ya ukaguzi wa vyeti feki hauwahusu watumishi wa kisiasa ambao ni wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na pamoja na Mawaziri, anaandika Dany Tibason.

Kairuki alitoa kauli hiyo jana wakati akikabidhi ripoti ya ukaguzi wa vyeti feki kwa watumishi hewa ambayo iliwasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli ambapo ukaguzi wa watumishi wote ni 435,000 bila kuwahusisha viongozi wa kisiasa.

Akikabidhi ripoti hiyo Kairuki amesema katika ukaguzi huo umefanyika kwa watumishi wa Umma huku serikali kuu haijaanza kukaguliwa.

Kiongozi huyo alieleza kuwa katika ukaguzi huo jumla ya watumishi ambao ni halali ni 37,600 huku watumishi 9,932 wamebainika kuwa wamegushi vyeti vyao.

Katika kutoa ripoti hiyo Kairuki alisema vyeti 1,538 vimekutwa vikiwa na majina zaidi ya mawili jambo ambalo limeonekana kuwa na utata ambayo yanafanana.

Akizungumzia juu ya kundi la vyeti vya taaluma, amesema jumla ya vyeti 11,396 vilionekana kuwa ni vya taaluma pekee bila kuambatanishwa na vyeti vya kidato cha nne wala kidato cha sita.

Akiwasilisha ripoti hiyo amesema kwa mujibu wa sheria mtu ambayo anabainika kugushi vyeti anatakiwa kupata adhabu ya kufungwa kifungo cha miaka saba.

Mawakala waliohusika na vyeti feki kukiona

Waziri huyo amesema pamoja na mambo mengine alitangaza kuwachukulia hatua kali mawakala ambao wamehusika katika kugushi vyeti na kulisababishia taifa hasara kubwa.

Prof. Ndalichako

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi. Prof. Joyce Ndalichako amesema kazi ya uhakiki siyo kazi nyepesi inatakiwa kufanyika kwa umakini mkubwa zaidi.

Mbali na hilo amesema alipendekeza kufanyika kwa ukaguzi katika watumishi wa sekta binafsi hususani katika sekta ya elimu na afya.

Waziri Mkuu anena

Muda mfupi baada ya kuwasirisha ripoti ya ukaguzi wa vyeti feki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akimkaribisha rais Dk. Magufuli amesema Serikali inakubaliana kabisa na mtu ambaye hakufikia kiwango kizuri cha elimu kujiendeleza na kufanya mitiani binafsi lakini siyo kuruka ngazi kwa kughushi vyeti.

“Serikali haijatoa ukomo wa kurudia utaini binafsi na hilo siyo kosa ila aliyeharakisha zaidi kwa kuruka ngazi hilo ndilo kosa” amesema Majaliwa.

JPM awafuta kazi wenye vyeti feki

Muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa vyeti rais Dk. Magufuli alitangaza kuwafukuza kazi watumishi, 9,932 ambao walibainika kugushi vyeti.

Pamoja na kutangaza kuwaachisha kazi watumishi hao pia ameagiza watumishi hao kutolipwa mshahara wao ambao walitakiwa kulipwa kwa mwezi ujao.

Amesema kwa wale wote ambao wamebainika kuwa wanatumia vyeti vya kugusi kuanzia leo, wanatakiwa kutokuwepo kazini huku hakisema mishahara yao isilipe na nafasi zao zitangazwe ili wenye sifa waweze kuomba.

“Sasa kuanzia sasa wale wote ambao ambao wamebainika kuwa wanatumia vyeti vya kugusi wasiendelee kuwepo kazini na wale ambao watajiondoa wenyewe wasichukuliwe hatua yoyote ila wale ambao watajifanya jeuri wapelekeni katika vyombo vya sheria ili waweze kufungwa kwa miaka saba” amesema Rais Magufuli.

Akizungumzia juu ya wale ambao wanavyeti vyenye utata aliagiza kusitishwa kwa mishahara yao hadi hapo utata utakapokuwa umetatuliwa.

Kwa upande wa wale waliowasilisha vyeti vya taaluma bila kuambatanisha vyeti vya kidato cha nne na sita wametakiwa kuendelea kulipwa mishahara yao huku utaratibu wa kuhakiki vyeti hivyo ukiendelea.

Amesema kwa watu wa taaluma wakati mwingine wamekuwa wakianzia ngazi ya chini hadi kufikia hatua ya kuwa wataaluma jambo ambalo wakati mwingine wanaweza kutokuwa na cheti cha kidato cha nne na sita na mkifanya haraka mtakuwa mmewakosea kweli kweli.

 

JPM ampiga kijembe JK

Katika hatua nyingine Rais Dk. Magufuli amempiga kijembe rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, kwa kueleza kuwa inashangaza kuona kuwa kuwepo kwa vyeti feki wakati mawaziri walikuwepo na makatibu walikuwa wapo pia.

“Viongozi wa awamu ya tano tunatakiwa kubadilika maana tumesema sana, tumelalamika sana, hivi wakati wa vyeti feki walikuwepo watu hawakuwaona, hatupo hapa kwa ajili ya kuwalaumu waliopita, bali tutambue dhambi walizizozifanya.

“Mawaziri hawakuwepo, Maktibu hawakuwepo au wakurugenzi hawakuwepo au nisema wapo?”alihoji Dk.Magufuli.

Katika hatua nyingine Rai Magufuli amesema yeye siyo mwananasiasa bali ni mtendaji hivyo hatahakikisha nchi ananaelekea kunatokatiwa.

“Bahati mbaya nchi imeshikwa na wanasiasa kulinda masilahi ya siasa, hata mimi lipipokuwa chuoni nilikuwa nawachukia sana wanasiasa wamekaa waongooo waoongo tu sasa mimi siyo mwana siasa lazima tusongo mbele tu” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!