Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama Kuu yamtoa Lijualikali gerezani
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama Kuu yamtoa Lijualikali gerezani

Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombelo (kushoto) ajidaliana na polisi wakati wa kesi yake
Spread the love

PETER Lijualikali (30), Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yupo huru. Amevuka vinzingiti dhidi ya haki. Ameshinda kesi ya rufaa ya jinai Na. 60 ya mwaka huu katika Mahakama Kuu, anaandika Pendo Omary.

Mbali na Lijuakali lakini dereva wake, Stephano Mgata (35), aliyehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita, naye yupo huru.

Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumuwa kifungo cha miezi sita jela.

Lijualikali na Mgata waliwakilishwa mahakamani na mawakili Tundu Lissu na Frederick Kihwelu huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili wa serikali, Faraja Nchimbi.

Kihwelu ameuambia MwanaHALISI Online mchana huu kwamba: “Sababu ya Lijualikali kushinda kesi ni hati ya mashtaka dhidi ya Lijualikali kutofautiana na maelezo ya mashtataka yaliyotolewa dhidi yake.

“Mh. Jaji alijielekeza kuangalia hati ya mashtaka. Ilikuwa na mapungufu mengi. Kubwa ni kwamba ilitofautiana na maelezo yalitolewa ya mashtaka. Hili ni takwa likisheria lazima hati ya mashtaka na maelezo vifanane. Hivyo ameamua kufuta hukumu,” anasema Kihwelu.

Hukumu dhidi ya Lijualikali ilitolewa Januari 11, 2017 na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro chini ya Hakimu Mkazi, Timothy Lyon, kwa kosa la “kufanya fujo na kusababisha taharuki” huku Stephano Mgata (35) ambaye ni dereva wake akiwa mshitakiwa wa pili akifugwa kifungo cha miezi sita nje.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!