May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lijualikali arudi uraiani, Sumaye ampokea

Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani (mwenye suti nyeusi) akiwa Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero (suti ya kaki) na wanachama wa Chadema wakitoka gerezani Ukonga

Spread the love

FREDERICK Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, ameongoza viongozi wa Chadema waliofika kwenye gereza la Ukonga kumtoa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali, anaandika Pendo Omary.

Lijualikali ametoka gerezani baada ya kushinda rufaa yake jana katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezo sita na mahakama ya Hakimu Mkazi Kilombero, Januari 11, 2017.

Sumaye alikuwa miongoni mwa vigogo wa Chadema ambao waliwasili gerezani hapo mapema leo asubuhi na kufuata taratibu za kumtoa mbunge huyo wa Kilombelo aliyekuwa anatumikia kifungo chake.

Viongozi hao wa Chadema wakiwa na mawakili wa Lijualikali waliofanikisha kushinda rufaa yake, walifanikiwa kumtoa mbunge huyo na kuendelea na shughuli nyingine.

error: Content is protected !!