Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Vyeti bandia vyazidi kutikisa
Habari MchanganyikoTangulizi

Vyeti bandia vyazidi kutikisa

Spread the love

WANANCHI wamewataka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, wabuni njia mbadala ya kudhibiti matumizi ya vyeti bandia katika mfumo wa utoaji elimu, anaandika Faki Sosi.

Hayo yamesemwa ikiwa ni siku chache baada ya serikali chini ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kuanzisha utaratibu mpya wa kuzuia wanafunzi wasio na vyeti vya kuzaliwa kutofanya mitihani ya darasa la nne na saba kwa lengo la kukomesha watumiaji wa majina na vyeti feki vya watu wengine.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo leo walipokuwa wakizungumza na MwanaHALISI Online ambapo kwa wakati tofauti wamesema kuwa vyeti vya kuzaliwa ni muhimu na serikali na mawakala wake walitakiwa kujua umuhimu wa jambo hili mapema.

Saidi Lubago mkazi Kinondoni, Dar es Salaam amesema kuwa Rita wangeweza kurekebisha mfumo wao wa utoaji vyeti.

“Itakuwa wamechelewa kwa sababu tayari wapo wangine watu wazima hawana vyeti vya kuzaliwa hivyo mfumo huo ungeanza mapema,” amesema Lubago.

Mariamu Hussein mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, amesema kuwa yupo yeye amepata usumbufu katika kutafuta cheti cha mtoto wake kutokana na watendaji wa Rita kutokamilisha zoezi hilo mapema ambapo yeye alishindwa kwenda kila siku kuhangaikia vyeti na kuacha kutafuta riziki.

Juzi, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Emmy Hudson alisema kuwa utaratibu huo mpya ni agizo la serikali lenye lengo la kuweka kumbukumbu sahihi za wanafunzi kuanzia ngazi ya chini na kukwepa udanganyifu wa majina na vyeti.

“Tayari juhudi mbalimbali zimechukuliwa ili kupunguza msongamano katika ofisi zao za kupata vyeti hivyo na tumeanza kuvitolea shuleni”.

Hivi karibuni kabla ya mfumo huo kutangazwa rasmi, kumekuwepo na taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia jina na cheti cha mtu mingine kujiendeleza kielimu huku jina lake halisi likielezwa kuwa ‘Daud Albert Bashite’.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!