Tuesday , 30 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

JPM amtaabisha Lissu

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, akilia kwa uchungu
Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi kuhusu kuwepo kwa njaa nchini, anaandika Faki Sosi.

Hatua hiyo inafuatiwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli kupinga kuwepo kwa njaa nchini na kwamba, wafanyabiashara wachache wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya watu kueneza taarifa hizo.

Simon Siro, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam leo amewaambia waandishi wa habari kwamba, wanamshikilia Lissu kutokana na tuhuma hizo.

Si mara ya kwanza Lissu ambaye ni Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukamatwa kwa madai yanayofanana na hayo.

Miongoni mwayo ni tarehe 22 Desemba mwaka jana ambapo Lissu aliachwa baada ya saa kadhaa kukamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kutumia jina la Rais Magufuli kwa dhihaka kwa kumwita rais mtukufu.

Alianza kuulizwa kuhusu mkutano wake na waandishi wa habari alipozungumzia kupotea kwa Ben Saanane, aliyekuwa msaidizi wa karibu wa Mbowe “aliitwa kuhojiwa juu ya Press conference aliyofanya na kuzungumzia suala la Saanane lakini pia wamemuhoji anamaanisha nini kumwita Rais John Magufuli jina la “Mtukufu.”

Lissu amekuwa akimtaja Rais Magufuli kama “mtukufu” mara kadhaa tangu aliposhitakiwa kwa kutamka kuwa “Dikteta uchwara anapaswa kupingwa kwa nguvu zote.”

Lissu alikamatwa jana jioni mjini Dodoma katika vianja vya bunge na kusafirisha moja kwa moja hadi jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukamatwa kwake, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa alieleza kutojua sababu za kukamatwa kwake.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa, Lissu anaendelea kuhojiwa kutokana na tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!