Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko MwanaHALISI yamalizana na JPM
Habari MchanganyikoTangulizi

MwanaHALISI yamalizana na JPM

Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI
Spread the love

UONGOZI wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), inayochapisha gazeti la MwanaHALISI, umemuomba radhi Rais Dk. John Magufuli, anaandika Faki Sosi.

Hatua hiyo imetekelezwa kupitia taarifa ya Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana.

Katika taarifa hiyo, Idrissa alisema wamejikuta na wajibu wa kumtaka radhi Rais, Serikali anayoiongoza pamoja na umma wa Watanzania kutokana na usumbufu uliotokea.

Mhariri Idrissa amesema habari iliyochapishwa kwenye toleo la juzi Jumatatu, chini ya kichwa cha maneno, “Ufisadi ndani ya Ofisi ya JPM” haikuleta taswira nzuri kwa Rais Dk. Magufuli kwa kuwa imeonekana ni kama ufisadi umefanyika ndani ya ofisi yake ambayo ni Ikulu (State House).

Idrissa amesema baada ya kurudia kusoma kwa uangalifu habari husika, amejiridhisha kuwa tafsiri iliyoibuka kuwa Rais anahusika na ufisadi huo si sahihi na hivyo kuna haja ya kuweka sawa.

“Kwa hakika nimeridhika na wenzangu katika uongozi wa gazeti wamenielewa kuwa rais hahusiki kwa sababu ofisi ya Rais inaishia Ikulu na sio Idara nyingine ikiwemo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitta (TAMISEMI),” amesema.

Alisema kwamba dhana kwamba Ikulu ni hata idara nyinginezo, haina usahihi kwa kuwa idara hizo zina mawaziri wake wanaozisimamia.

“Nimejirudi baada ya kufanya majadiliano marefu na Msajili wa Magazeti ambaye kwa kweli amenisaidia kuelewa kwa undani hisia zilizomjaa Rais kutokana na habari tuliyoichapisha. Tunamuomba radhi kwa hilo.

“Sasa kwa nafasi yangu ya Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI, baada ya hatua ya kujirudi, niache akiba kwamba ni jukumu la serikali kuchukua hatua kwa kile tulichokusudia umma ukielewe ya kwamba hatua zichukuliwe dhidi ya ufisadi huo,” alisema Idrissa.

Juzi serikali kupitia Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas alitoa taarifa ya kumtaka Mhariri wa MwanaHALISI kumuomba radhi Rais kwa kosa la kumhusisha na ufisadi uliofanywa katika Shirika la Elimu Kibaha (SEK) tangu mwaka 2014.

Dk. Abbas alisema habari husika imejenga dhana kuwa Wizara ya Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambako shirika hilo linawajibika kiuongozi, inaihusu Ikulu wakati sivyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!