
Kikosi cha Memelodi Sundown
KLABU ya Azam FC leo itashuka dimbani dhidi ya mabingwa Klabu Bingwa Afrika, Mamelodi Sundown katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa majira ya saa moja jioni, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, anaandika Kelvin Mwaipungu.
Mamelodi ambao wameingia nchini siku ya Jumatatu kwa ajili ya ziara maalumu, sambamba na kufanya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Febuari 18 mwaka huu.
Licha ya kucheza na Azam FC leo, klabu hiyo pia itacheza mchezo mwengine siku ya Ijumaa dhidi ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam kabla ya kurudi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya CAF.
More Stories
Yanga yaanza safari ya kutetea ubingwa wake
Ngao ya Jamii kuchezwa kwa mtoano
KMC yatua Arusha kibabe