Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Tunda Man azishauri shule kuwa na programu za kuibua vipaji
ElimuMichezo

Tunda Man azishauri shule kuwa na programu za kuibua vipaji

Spread the love

 

MWANAMUZIKI Khaleed Ramadhan maarufu kama Tunda Man alifanya onyesho la aina yake kwenye shule ya Brilliant na kuzishauri shule ziwe na profamu za kuibua vipaji vya vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu…..(endelea)

Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akitumbuiza kwenye mahafali ya shule ya sekondari ya Brilliant ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

Alisema mbali na masomo kuna umuhimu kwa shule kutenga muda wa michezo na burudani kwani kwa kufanya hivyo wataibua vipaji vingi na watu maarufu kwa siku za usoni.

Tunda Man aliibua shangwe kwa wanafunzi wa shule hiyo mara tu mshereheshaji wa tukio hilo alipotangaza uwepo wake kwenye mahafali hayo.

Aliposhuka kwenye gari lake wanafunzi walishindwa kujizuia na wote walivamia katikati ya uwanja na kuanza kuimba naye nyimbo mbalimbali ukiwemo ule wa naipenda Simba hatua uniue mimi sihami.

Tunda mbali na kuimba wimbo maarufu wa naipenda Simba sihami hata mniue aliimba nyimbo mbalimbali za kupongeza mafanikio ya timu ya Yanga hali iliyoibua furaha na shangwe kwa wanafunzi wa timu zote mbili.

Aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha nne inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

error: Content is protected !!