Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yavunja ukimya mchakato katiba mpya, kutoa elimu kwa miaka 3
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yavunja ukimya mchakato katiba mpya, kutoa elimu kwa miaka 3

Spread the love

SERIKALI imevunja ukimya kuhusu utekelezaji mchakato wa marekebisho ya katiba, ikisema kwa sasa imeweka kipaumbele katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu suala hilo, zoezi litakalofanyika kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia 2023 hadi 2026.Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 28 Agosti 2023 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro, akizungumza katika kikao cha mawaziri wa sheria na wanasheria wakuu wastaafu na waliopo madarakani, kuhusu majadiliano ya katiba mpya na mkakati wa taifa wa elimu ya katiba ya 1977 kwa umma (MTEKU 2023/26).

Dk. Ndumbaro amesema kuwa, Serikali imeweka kipaumbele juu ya suala hilo, baada ya kubaini kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wananchi hawaifahamu katiba na majukumu yake, kitendo alichodai kinapelekea baadhi ya wanasiasa kuwaongoza vibaya.

“Kwa mwaka huu tumeweka kama kipaumbele namba moja kwa sababu kuna tafiti kadhaa zimefanyika na zimebainisha kwamba zaidi ya asilimia 50 ya watanzania hawaifahamu katiba. Wengine wanasema hata kuiona hawajaiona. Sasa chukulia umuhimu wa katiba katika jamii yoyote, hivyo tunawajibu kuhakikisha wanaifahamu,” amesema Dk. Ndumbaro.

Waziri huyo wa katiba amesema “hatari ni kwamba wasipoifahamu watachukulia yale wanayoambiwa yasiyo ya kweli kuhusiana na katiba wakaamini. Mfano mwaka jana bei za vyakula zilipanda kuna mtu mmoja msomi anaongea kwamba bei zimepanda tatizo ni katiba, kwa hiyo tunataka katiba mpya bei zishuke, inawezekana sisi tusikubaliane na hilo sababu tuna uelewa lakini kuna watu wataamini ugumu wa maisha inatokana na katiba yetu siyo nzuri.”

Dk. Ndumbaro amesema hadi sasa kuna mjadala juu ya hatua gani ambayo inatakiwa kuanza pindi mchakato huo utakapofufuliwa, ikiwemo kama kuanzia mchakato wa kura ya maoni dhidi ya rasimu ya katiba pendekezwa, ukusanyaji wa maoni mapya kuhusu marekebisho hayo au utungwaji sheria ya katiba na Bunge litakalousimamia.

Pia, Dk. Ndumbaro amesema mvutano uliopo kuhusu suala hilo, ni kama katiba yote ifumuliwe na kuandikwa upya, au iliyopo irekebishwe katika baadhi ya vifungu vinavyoonekana vina dosari.

“Lakini wapo wanaosema tutunge sheria ya mabadiliko ya katiba na tuunde Bunge la katiba tuanzie hapo, tusonge mbele. Wako ambao wanasema kutoka tulipochukua maoni ya mara ya mwisho,”

“Mpaka sasa zaidi ya miaka 10 mengi yamejitokeza hapo ambao watanzania hawakuyajua kwa wakati ule hivyo ni vizuri tuwape nafasi ya kusema kidogo na wanawake mkazo wanasema kuna vijana wakati huo walikuwa chini ya umri wa miaka 18 sasa wamevuka na wako asilimia 30 ya idadi ya watanzanioa wanasema lazima washirikishwe,” amesema Dk. Ndumbaro.

Amesema mchakato wa katiba lazima uridhiwe na pande zote kwa kuwa suala hilo linahitaji kuwa na uhalali.

“Mmoja alinipa ujumbe kwamba waziri sisi hatutaki jambo lolote tunataka ufufue mchakato pale tulipoishia twende kura ya maoni, nikamuuliza tuliishia wapi akasema tulipitisha ile rasimu katiba pendekezwa, nikawambia nafahamu unatoka chama fulani akasema kweli. Wewe na chama chako mbona mlisusa?” amesema Dk. Ndumbaro na kuongeza:

“Moja kati ya msingi ya katiba ni uhalali wa katiba, nikamwambia kitendo kile cha ninyi kususia na kutoka nje kilitia doa kwenye uhalali wa ule mchakato, labda kama leo mtatuambia kwamba yale yalikuwa maigizo sasa mmeyaacha twende pale, hakuwa na jibu kwenye hilo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!