Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Nimedhulmiwa ushindi wa Urais– Chamisa
Kimataifa

Nimedhulmiwa ushindi wa Urais– Chamisa

Spread the love

MPINZANI katika uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa amelalamika kudhulumiwa haki yake ya kushinda kuwa Rais wa Zimbabwe dhidi ya Emmerson Mnangagwa kwenye uchaguzi uliofanyika kuanzia tarehe 23 Agosti 2023. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

 Hayo yamejiri baada ya tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Zimbabwe (ZEC) kumtangaza Mshindi wa uchaguzi huo Rais Emmerson Mnangagwa kushinda kiti hicho kwa mara ya pili kwa asilimia 52.6 ya kura zote.

Mshindi wa pili wa Uchaguzi huo Nelson Chamisa kutoka chama cha Citizens’ Coalition for Change (CCC) aliyeshinda kwa asilimia 44 amelalamikia kwa waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU OEM) kunyanganywa ushindi huo

Akizungumza baada ya matokeo hayo Chamisa ameeleza kutoridhishwa na matokeo hayo

“Tulijua tunaingia kwenye uchaguzi wenye dosari. Tuna orodha ya wapiga kura yenye dosari, ripoti yenye dosari. Tulikuwa na kura yenye dosari. Yalikuwa mazingira ya uchaguzi yenye dosari,” alisema Chamisa.

Pia ameeleza kuwa Chama chake kimeshinda uchaguzi huo na haikuwa sahihi Tume ya uchaguzi kumtangaza Mnangagwa kuwa Rais.

“Tumeshinda uchaguzi huu. Sisi ni viongozi. Tunashangaa hata kwa nini Mnangagwa ametangazwa kuwa kiongozi,” Chamisa, wakili na mchungaji anayeongoza chama cha CCC, aliwaambia waandishi wa habari leo Jumatatu katika mji mkuu Harare.

Katika hatua nyingine Mwanahakati Runtendo Rutenyarare kutoka chama cha ZANU PF amesema Chamisa atakuwa amekiuka sheria za uchaguzi kama atashindwa kuthibitisha tuhuma zake dhidi ya Rais Mnangagwa na Tume ya uchaguzi.

“Kama Chamisa na viongozi wengine wa CCC wanadai kuwa uchaguzi uliibiwa lakini wakashindwa kuthibitisha wizi mahakamani, basi ina maana kwamba:

“Kwanza, waliwasilisha taarifa ambayo walijua kuwa ni ya uongo na hawakuwa na msingi wa kuamini kuwa ni kweli, waliiwasilisha kwa hadhira ya kimataifa kwa nia ya pamoja na mambo mengine, wakichafua taswira ya Zimbabwe kushawishi wawekezaji kususia Zimbabwe au kuiwekea Zimbabwe vikwazo, kwa faida yao.

“Hii ni kinyume cha kifungu cha 22A (4) (b) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (codification and amendment),” anasema Runtendo.

Rais Mnangagwa baada ya tuhuma hizo amesema kuwa yeyote ambaye anahisi kuwa uchaguzi haukuwa wa haki basi aende mahakamani.

Pia amewashukuru wananchi wote kwa kuonesha ushirikiano wakati wote wa uchaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!