Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara DC Same atoa mwezi mmoja halmashauri kuhamisha gulio
Biashara

DC Same atoa mwezi mmoja halmashauri kuhamisha gulio

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa halmashauri hiyo kuhamisha gulio linalofanyika Jumatano hadi Jumapili eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanja vya michezo maarufu Kwasa-Kwasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Same ambapo amesisitiza uboreshwaji wa miundombinu kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.

Alisema kitendo cha halmashauri kuruhusu eneo la michezo kutumika kama gulio hakikubaliki kwani kinarudisha nyuma jitihada za serikali kukuza michezo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema wanamichezo wamekuwa wakilalamika ila hawasikilizwi hivyo anatoa mwezi mmoja kwa halmashauri kupata ufumbuzi wa kero hiyo.

Aidha, Kasilda ameeleza kutoridhishwa na hali ya Soko Kuu la Mji wa Same kutokana na uchafu uliokithiri, vyoo vinavyotumika kukosa ubora unaohitajika hivyo kuhatarisha usalama wa afya za wafanyabiashara na wanunuzi wanaotumia soko hilo na kuagiza halmashauri kukarabati haraka iwezekanavyo.

Awali wafanyabiashara wa soko hilo wakitoa malalamiko yao wamemweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa soko hilo linakabiliwa na ubovu wa miundombinu, kama mashimo makubwa yaliyo ndani ya soko, kukosekana umeme hali inayosababisha kuendesha biashara kwa shida wakitaharisha pia usalama wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!