Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yahofia mkwamo mageuzi kisiasa
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yahofia mkwamo mageuzi kisiasa

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo, imeitaka Serikali kutoa ratiba ya utekelezaji wa mageuzi ya kisiasa nchini. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 28 Agosti 2023 na Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria wa ACT-Wazalendo, Mbarala Maharagande, akitoa taarifa ya uchambuzi wa kamati ya kusimamia Serikali ya wasemaji ya kisekta (Baraza Kivuli), ya chama hicho, juu ya majadiliano yanayoendelea kuhusu mageuzi ya kidemokrasia.

Taarifa ya Maharagande imesema kuwa, ACT-Wazalendo inapata wasiwasi kwenye utaratibu wa utekelezaji wa maoni na maeneo yaliyofikiwa mwafaka na wadau, kutokana na mjadala huo kuchukua muda mrefu bila ya kuwa na kalenda ya utekelezaji.

“Tangu mwaka jana, tumekuwa tukitoa wito kwa Serikali kuweka ratiba ya kila jambo na namna utekelezaji wake. Hivyo basi, tunarudia tena wito wetu kuwa tunaitaka Serikali iweke wazi ratiba ya utekelezaji wa maazimio ya wadau kutoka majukwaa mbalimbali ili kuwa na sheria mpya ya vyama vya siasa sheria mpya ya uchaguzi na marekebisho ya Sheria ya mchakato wa Katiba mpya,” imesema taarifa ya Maharagande.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimewata wadau wengine kushirikiana kwa pamoja kuitaka Serikali kuanza kutekeleza maazimio yatakayoleta mageuzi ya uendeshaji wa siasa.

“Tarehe 22 na 23 Agosti 2023, wadau wa siasa kupitia jukwaa la Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), walikuwa na majadaliano yaliyowezesha kupata mwafaka kwenye masuala kadhaa, kuhusu mageuzi yanayopaswa kufanyika katika uendeshaji wa siasa zetu nchini,” imesema taarifa ya Maharagande na kuongeza:

 

“Kufuatiwa na mjadala huo, tumeona kwa sasa upo mwafaka kwa wadau wote juu ya madai ya kuwa na Tume huru ya uchaguzi, kuanza kwa mchakato wa katiba mpya, mabadiliko ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa na mabadiliko ya vyombo vinavyohusika na usimamizi wa siasa (Sheria ya Jeshi la Polisi).”

Wito huo wa ACT-Wazalendo, umekuja katika kipindi ambacho wadau wa demokrasia ya vyama vingi, wanaishinikiza Serikali kufanya marekebisho ya sheria zinazosimamia tasnia hiyo na katiba, kabla ya chaguzi zijazo ili ziwe huru na za haki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!