Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Balozi atoa ufafanuzi binti Sayuni kutimuliwa ubalozini India
Habari Mchanganyiko

Balozi atoa ufafanuzi binti Sayuni kutimuliwa ubalozini India

Spread the love

Ubalozi wa Tanzania nchini India umetoa ufafanuzi kuhusu Mtanzania, Sayuni Eliakim aliyedaiwa kushindwa kusaidiwa ubalozini hapo kupata hati ya kusafiria ili arudi Tanzania, kwamba muda wake wa ukaazi katika nchi hiyo ulikuwa umeisha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ufafanuzi huo umekuja siku mbili baada ya taarifa zilizodai Sayuni aliyedaiwa kunyanyang’anywa hati ya kusafiria na mwenyeji wake nchini humo kuwa alikosa huduma ubalozini hapo na kumtaka arudi ajaze maombi hayo kwa njia ya mtandao.

Taarifa ya Balozi wa Tanzania nchini India, Anisa Mbega aliyoitoa leo tarehe 28 Agosti 2023 kupitia mtandao wa Twitter, amesema anapenda kutoa taarifa sahihi kuhusu Sayuni Eliakim, aliyefika Ubalozini tarehe 26 Agosti 2023, kuomba msaada wa kurejeshwa nyumbani nchini Tanzania.

Amesema Sayuni aliingia nchini India mwaka 2018, na kukaa kwa muda mrefu hadi kujikuta muda wake wa ukaazi umepita.

Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uhamiaji za India, raia wa kigeni ambaye amepitisha muda wake wa ukaazi, haruhusiwi kutoka nchini India, isipokuwa kwa utaratibu maalum uliowekwa.

“Utaratibu huo ni pamoja na kuomba ruhusa ya kutoka nje ya nchi (Exit Permit). Maombi ya Exit Permit yanatakiwa kufanyika katika mji ambao Mhusika anaishi (kwa upande wa bi. Sayuni mji anaoishi ni Bangalore).

“Sayuni alielekezwa kuhusu utaratibu huo na maombi yake hadi hivi sasa yanaendelea kufanyiwa kazi. Ubalozi unaendelea kumsaidia Sayuni ikiwemo kumpatia Hati ya kusafiria ya dharura (ETD),” amesema.

Aidha, amesema Ubalozi utahakikisha kuwa suala lake linapatiwa ufumbuzi kama ambavyo imefanyika kwa Watanzania wengine kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Ameongeza kuwa kuanzia mwezi Juni hadi Agosti 2023, Ubalozi umewapokea, umewaelekeza na kuwapa msaada Watanzania wapatao 60 na hivi sasa wamerejea nyumbani kuungana na familia zao nchini Tanzania kwa utaratibu huo huo ambao Sayuni alipewa.

Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini India unapenda kusisitiza kuwa Watanzania wote wanaofika Ubalozini wanahudumiwa kwa haki na usawa bila ubaguzi wa aina yoyote, kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na nchi mwenyeji.

“Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Ubalozi unalisimamia vizuri suala la Sayuni na kwa kushirikiana na ndugu zake tutahakikisha Sayuni anarejea salama nyumbani Tanzania na kuungana na familia yake.

“Ubalozi unatoa rai kwa Watanzania kujiepusha na kuchukua tahadhari na watu wasio waaminifu wanaowalaghai kuhusu kuwepo kwa nafasi za ajira zisizo na ujuzi kwa raia wa Tanzania nchini India,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!