Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara NBC yashiriki ‘Wogging’ ya AMREF, yakabidhi msaada wa Mil. 200
Biashara

NBC yashiriki ‘Wogging’ ya AMREF, yakabidhi msaada wa Mil. 200

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wadau wengine kushiriki kwenye mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la AMREF -Afrika, tawi la Tanzania zikilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kupitia tukio hilo ambalo ni sehemu ya kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shs 200 milioni vitakavyotumika kwenye hospitali mbalimbali za Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya visiwani humo.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa tayari kuongoza washiriki wa mbio fupi zilizo ambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. Pamoja nae pia wapo Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh (kushoto kwa Rais Mwinyi), Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais Mwinyi) na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (Kushoto kwa Naibu Hafidh)

Akizungumza mara baada ya kushiriki matembezi hayo yaliyoanzia eneo la Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar mwishoni mwa wiki, Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali Benki ya NBC, Linley Kapya alisema mbali na mazoezi ya viungo, ushiriki wa benki hiyo ulilenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza na kuepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ambapo bado kiwango cha changamoto hiyo kipo juu.

‘’Kama ambavyo amebainisha Rais Dk. Mwinyi kwamba takwimu zinaonesha kuna vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017. Hali hiyo husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu na tatizo la kukosekana kwa dawa.’’

‘’NBC tukiwa wadau tunaosapoti sekta zote ikiwemo michezo na afya tukaona ni vema kwetu tukiwa sehemu ya jitihada hizi muhimu,’’ alisema.

Maofisa wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wateja wa serikali wa benki hiyo Linley Kapya (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu (wa pili kushoto) mara baada ya kukabidhiwa chetu cha shukrani na utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kampeni ya ‘Uzazi na Maisha’ iliyoambatana na mbio fupi zilizoambatana na matembezi ya hiyari (Wogging) zilizofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki. 

Kwa mujibu wa Kapya mbali na michezo, Benki hiyo imekuwa mdau mkubwa wa Afya visiwani humo ambapo imekuwa ikitoa huduma za vipimo bure kwa wamama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kupitia program yake ya Mobile Clinics kwa kushirikia na Wizara ya Afya ya Zanzibar.

Akizungumza kwenye tukio hilo pamoja na kuzungumzia umuhimu wa mazoezi kiafya sambamba na kuwapongeza washiriki wa wogging hiyo, Dk. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba Serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vyote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya “Uzazi ni Maisha” inayohusisha michezo ni kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini.

Naye, Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Amref Afika Tanzania, Dk. Florence Temu pamoja na kuwashukuru wadau mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni hiyo pamoja na wanamichezo walioshiriki wogging hiyo, alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ya “Uzazi ni maisha ni kukusanya shilingi Bilioni moja kwajili ya kununuliwa vifaa tiba vya hospitali na vituo vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.

‘’Tukiwa kwenye mwaka wa pili wa kampeni hii, Shirika la Amref tayari tumefanikiwa kukusanya milioni 557 na tumepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hii kufikia 2024.’’ Alibainisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!