Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanroads yatakiwa kuharakisha ujenzi wa barabara Kidatu-Kilombero
Habari za Siasa

Tanroads yatakiwa kuharakisha ujenzi wa barabara Kidatu-Kilombero

Barabara ya kiwango cha rami
Spread the love

KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameisisitiza Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kumsimamia kikamilifu mkandarasi anaye jenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kidatu – ifakara yenye urefu wa kilomita 66.9 ili aweze kukamilika kazi kwa muda sahihi uopangwa na Serikali na kuanza kutumika kwa manufaa ya wakulima na wafanyabiashara. Anaripoti Christina Haule, Kilombero … (endelea). 

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuwasili wilayani Kilombero kutokea wilayani Kilosa Chongolo alisema haiwezekani ujenzi huo uchelewe wakati fedha za utekelezaji wake tayari zilishatengwa na kuonya wasimamizi watakao kaidi maelekezo hayo ya chama.

Hata hivyo alimtaka mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa kukaa na viongozi wa vyama vya wakulima AMCOS ili kuona namna ya kuwapa elimu ya namna ya kuzalishwa miwa yenye kiwango kikubwa Cha Sukari ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa utamu kwenye miwa.

Naye Mbunge wa jimbo la Kilombero Aboubakar Assenga aliiomba TANROADS kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kuwasaidia wakulima kwa kurahisisha usafirishaji wa bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Alisema wilaya hiyo inayojishugulisha na kilimo ikiwa na uwekezaji wa viwanda vya Sukari Kilombero na Ilovo inakabiliwa na changamoto za utamu kwenye sukari, barabara na Soko la bidhaa zao ambalo aliahidi kulipatia ufumbuzi mapema.

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM

Akizungumza kwenye kikao hicho mbunge wa jimbo la Mikumi Denis Londo aliishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango Cha lami ili kurahisisha mawasiliano kati ya Wilaya ya Kilombero na Kilosa kupitia daraja la kidatu ambalo nalo limefanyiwa marekebisho maboresho.

Naye Meneja wa TANRODS mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alisema Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango Cha lami ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 kwa gharama ya shilingi  Bilioni 105.035 za Tanzania ambapo inatarajiwa kukamilika Oktoba 2023.

Alisema utekekezaji wa mradi huo katika kipindi Cha Januari Hadi Desemba mwaka 2022 imezalisha ajira 903 ambapo kati ya hizo ni wanawake 191 na wanaume 712.

Aidha alisema katika kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo Serikali ililipa fidia kiasi cha sh bil 2.6 kwa waathirika mbalimbali mwaka 2018 na mwaka 2019.

Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mhandisi Fadhili Chilombe alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!