September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania, Kenya zaungana kulinda rasilimali za mipakani

Spread the love

SERIKALI ya Kenya na Tanzania zimeungana kwa pamoja kulinda rasilimali za asili zilizoko katika mipaka ya nchi hizo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter jana tarehe 15 Januari 2019, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba ameandika kuwa, makubaliano hayo aliyasaini yeye pamoja na Waziri wa Mazingira na Misitu wa Kenya, Keriako Tobiko tarehe 29 Novemba 2018.

January ameandika kuwa, katika utekelezaji wa makubaliano hayo, wataangalia namna bora juu ya uhifadhi wa mazingira hasa katika maziwa ya Chala, Jipe, Natroni na Mto Mara.

Mambo mengine yatakayotekelezwa katika makubaliano hayo ni pamoja na uundwaji wa kamati ya pamoja kwa ngazi ya wizara ili kuratibu shughuli za usimamizi rasilimali za asili zilizoko mipakani, pamoja na kuanzisha timu ya wataalamu ili kutoa muongozo wa kiufundi katika usimamizi wa mipaka.

error: Content is protected !!