September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Nimejiuzulu Chadema kulinda maisha yangu’

Bendera ya Chadema

Spread the love

RAPHAEL Mwaitege, Katibu wa Chadema wilayani Mbeya Mjini amejivua uanachama pamoja na nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya chama hicho, kwa ajili ya kunusuru maisha yake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwaitege ametangaza uamuzi huo leo tarehe 15 Januari 2019 wakati akizungumza na wanahabari na kudai kwamba, baadhi ya wanachama wenzake wamekuwa wakimtishia maisha yake.

Kutokana na vitisho hivyo, Mwaitege amesema ameamua kupumzika siasa. Hata hivyo, Mwaitege amesema amevutiwa na sera za chama cha CCM.

error: Content is protected !!