Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Twitter yamfungia kabisa Rais Donald Trump
Kimataifa

Twitter yamfungia kabisa Rais Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump
Spread the love

AKANUTI ya Twitter ya Rais wa Marekani, Donald Trump imefungiwa kabisa, kutokana na hatari ya kuitumia kuchochea vurugu nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa ya kampuni hiyo imesema, uamuzi huo umefikiwa baada ya kufuatiliwa kwa karibu jumbe za Twitter zinazowekwa kwenye akaunti ya @realDonaldTrump.

Baadhi ya wabunge na watu mashuhuri wengine mashuhuri nchini Marekani, wamekuwa wakitoa wito kwa miaka mingi, kwa mtandao wa Twitter kuzuia akaunti ya Bwana Trump.

Michelle Obama, alliyekuwa mama wa taifa la Marekani aliandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter, Alhamisi iliyopita akisema, kituo cha ubunifu wa teknolojia duniani, Silicon Valley kinastahili kuzuia uendelezaji wa tabia mbaya za Bwana Trump na kumfuta kabisa kama mtumiaji wa huduma hizo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza (BBC), Rais Trump alifungiwa akaunti yake ya Twitter kwa saa 12 Jumatano iliyopita, baada ya kutoa wito kwa wafuasi wake kuvamia Bunge ambao aliwaita “wazalendo.”

Mamia ya wafuasi wake walivamia Bunge wakijaribu kuvuruga kikao cha kuidhinisha ushindi wa rais mteule, Joel Biden kama rais. Vurugu hizo zilisabbaisha vifo vya raia wanne na afisa mmoja wa polisi.

Mtandao wa Twitter baadaye ukaonya kuwa unaweza kumpiga marufuku Bwana Trump kuutumia kabisa ikiwa atakiuka tena kanuni za jukwaa hilo la mawasiliano.

Baada ya akaunti yake ya Twitter kuwezeshwa tena, Bwana Trump alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Ijumaa na kusema:

“Wamarekani 75,000,000 Wazalendo walionipigia kura, Marekani Kwanza na Fanya Marekani kuwa Bora Tena, watakuwa na sauti inayosikika siku zijazo. Hawatakosewa heshima au kuchukuliwa kwa uonevu kwa namna yoyote ile!!!”

Mtandao wa Twitter umesema, ujumbe huo “umeutafsiri kama ishara zaidi ya kuwa Rais Trump hana mpango wa kuhakikisha kunafanyika ‘mabadilishano’ ya madaraka kwa njia ya amani.”

Katika ujumbe mwingine rais aliandika: “Kwa wote ambao wameuliza, sitahudhuria hafla ya kuapishwa Januari 20.”

Mtandao wa Twitter umesema kuwa ujumbe huo “umechukuliwa na wafuasi wake kadhaa kama thibitisho la kwamba uchaguzi huo haukuwa halali.”

Mtandao wa Twitter umesema, ujumbe wote huo alioandika, “unakiuka sera na kanuni katika uhamasishaji wa vurugu.”

Baada ya akaunti yake ya @realDonaldTrump kufungwa kabisa, Trump alituma ujumbe kwa kutumia akaunti rasmi ya rais wa Marekani @Potus akisema kuwa “ataangalia uwezekano wa kuwa na mtandao wao utakaowezesha mawasiliano siku za usoni” na kukosoa Twitter.

Hata hivyo, ujumbe wake ulifutwa katika jukwaa hilo la mawasiliano muda mfupi baada ya kuwekwa.

Donald Trump’s tweets from @POTUS account, 8 January 2021

Akijibu baada ya kupigwa marufuku, mshauri wa kampeni ya Trump 2020, Jason Miller ameandika kwenye Twitter: “Inachukiza… ikiwa hujafikiria kwamba wewe ndio wa pili watakaekufuata, umekosea.”

Kwanini Twitter ulikuwa mtandao maarufu sana kwa Trump?

Bwana Trump alitumia mtandao wa Twitter kutukana wapinzani wake, kushabikia washirika wake, kuwafuta kazi maafisa, kukanusha “taarifa za uongo” na kutoa malalamishi yake, mara nyingi akiandika kwa kutumia herufi kubwa na alama za mshangao kusisitizia anachozungumzia.

Ingawa wakosoaji wake wamesema mara nyingi ujumbe wake ulikuwa wa kupotosha, mtandao huo ulimsaidia kukabiliana na mengi na aliweza kwa haraka, kuwasiliana na wafuasi wake karibu milioni 89.

Aidha, mara kadhaa jumbe zake, zilikuwa na makosa ya herufi na wakati mwingine aliacha wafuasi wake kukisia tu kile alichomaanisha.

Idara ya sheria ilisema mwaka 2017 kuwa ujumbe wa Bwana Trump ulikuwa “mawasiliano rasmi ya Rais wa Marekani.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!