May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndege yenye abiria 62, yapotea

Spread the love

NDEGE ya Kampuni ya Sriwijaya Air, aina ya Boeing 737 imepoteza mawasiliano na haijulikani ilipo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Taarifa zinaeleza, ndege hiyo iliyokuwa na takribani abiria 62, ilipoteza mawasiliano yake muda mfupi baada ya kuondoka katika Uwanja wa Jakarta, Indonesia ikielekea Pontianak magharibi mwa eneo la Kalimantan, nchini humo jana Jumamosi tarehe 9 Januari 2021.

Taarifa za mtandao unaofuatilia safari za ndege Flightradar24.com zimeeleza, ndege hiyo ilipoteza mawasiliano baada ya kupaa mita 3,000 ndani ya dakika moja.

Hata hivyo, mvuvi mmoja amesema, alisikia mlipuko mkubwa baharini.

Amesema, “ndege hiyo ilianguka kama radi ndani ya bahari na kulipuka ndani ya maji,” na kuongeza: “Ilikuwa karibu sana na sisi na vipande vya mfano wa mbao nyepesi karibu vipige meli yangu.”

Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa zaidi ambapo Wizara ya Usafirishaji Indonesia imesema, shughuli za utafutaji na uokozi wa ndege hiyo zinaendelea.

Wizara hiyo imesema, mawasiliano ya mwisho na ndege hiyo yalifanyika 14:40 saa za Indonesia.

Kwa mujibu wa taarifa za usajili wa ndege hiyo aina ya Boeing 737-500, imekwisha kutumika kwa miaka 27.

Inaelezwa, baadhi ya waliokuwepo ndani ya ndege ni watoto saba na wachanga watatu- wahudumu wa ndege 12 ingawa ndege yenyewe ina uwezo wa kubeba watu 130.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!