Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu akamatwa tena
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu akamatwa tena

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki (katikati) akiwa chini ya ulinzi alipokamatwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni
Spread the love

JESHI la polisi limemkamata mwanasiasa machachari nchini na mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, anaandika Saed Kubenea.

Lissu ambaye amepitishwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kugombea nafasi ya urais, amekamatwa na polisi asubuhi hii (Alhamisi, 16 Machi), nyumbani kwake mjini Dodoma.

Akizungumza kwa njia ya simu kabla ya kukamatwa, Lissu amesema, “…kuna askari wamenifuata hapa nyumbani kwangu kutoka ofisi ya mkuu wa polisi wa mkoa (RPC). Wametumwa kuja kunikamata.”

Anasema, “Sijajua kosa langu kwa kuwa sijazungumza nao. Lakini bila shaka wamekuja kunikamata, ili nisiweze kushiriki uchaguzi mkuu wa chama cha mawakili. Wanataka nisichaguliwe kuwa rais wa mawakili wenzangu.”

Lissu ambaye ni wakili wa mahakama kuu na mmoja wa watetezi wakubwa wa haki za kiraia, anasema kuwa wakati anafuatwa na askari hao alikuwa mbioni kuelekea mahakamani kusikiliza uamuzi wa shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu mjini Dodoma.

Kesi ambayo Lissu anasema alikuwa anakwenda kuhudhuria, inahusu maombi ya kuzuia uchaguzi wa chama hicho.

“Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi kutaka kunizuia kuwa rais,” ameeleza.

Baadaye akiandika kwa mawakili wenzake na marafiki wengine, Lissu alisema yafuatayo:

Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.

Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado, lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye uchaguzi wa TLS.

Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi. Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania, nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia.

Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii. Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama?

Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.

Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu, ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu.

Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene.

Msikubali kuyumbishwa. Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu. Nawatakieni kila la kheri. I’ll think of you all wherever they’ll take me to, wherever I’ll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has.

Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences. All the best.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!