August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi TLS, Dk. Mwakyembe aanza kupukutika

Harrison Mwanyembe, Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania

Spread the love

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, siyo mjumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) na hivyo hataweza kupiga kura, anaandika Saed Kubenea.

Dk. Mwakyembe ambaye ni wakili wa mahakama kuu, hataruhusiwa kupiga kura kwa kuwa hayumo kwenye orodha ya mawakili walioidhinishwa na Jaji mkuu kwa mwaka huu.

Taarifa zinasema, Dk. Mwakyembe hakuidhinishwa kuwa wakili kutokana na kushindwa kulipa ada zake za kila mwaka kama ilivyoekezwa na sheria za nchi na kanuni za TLS.

Katika siku za hivi karibuni, Dk. Mwakyembe amekuwa akitoa kauli tata kupinga chama hicho kupitisha wagombea anaodai ni wanasiasa na kusema, “hilo likitokea, serikali haitasita kuifuta TLS.”

Dk. Mwakyembe hajamtaja mwana taaluma ambaye ni mwanasiasa na ambaye anataka kugombea urais wa chama hicho.

Hata hivyo, anayeonekana kulengwa na Dk . Mwakyembe, ni Tundu Lissu, wakili machachari nchini, mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrsia na Maendeleo ( Chadema).

Lissu, ni miongoni mwa wagombea wanne wa wanafasi ya Rais wa TLS.

error: Content is protected !!